Matukio Picha Katika Maandamano Kupinga Utekaji wa Wasichana Nigeria

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (aliyeshika kipaza sauti) akisoma barua maalumu iliyotumwa kwa ubalozi wa Nigeria nchini Tanzania kuonesha wanaharakati hao kupinga utekaji wa wasichana uliofanyika Nigeria.

Mkurugenzi wa WiLDAF, Dk. Judith Odunga, akizungumza kupinga ukatili uliofanywa kwa wanafunzi wa kike kutekwa na kitendo cha Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuzuia maandamano hayo ya wanaharakati.

Viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea mabango yenye jumbe anuai za kupinga vitendo vya kikatili vilivyofanywa  na wanamgambo wa Boko Haram.

Baadhi ya wanafunzi wa kike na wanaharakati wakiandamana kupinga vitendo vya kikatili vinavyofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.

Baadhi ya wanaharakati na wanahabari wakisikiliza sauti za viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) mara baada ya kupokea maandamano ya wanaharakati na wanafunzi kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa na huzuni kwenye maandamano hayo.

Mkurugenzi wa WLAC, Theodosia Muhulo (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika mkutano na  wanahabari mara baada ya maandamano ya Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) na wanaharakati wengine kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram.

Mkurugenzi wa WLAC, Theodosia Muhulo (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika mkutano na
wanahabari mara baada ya maandamano ya Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) na wanaharakati wengine kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram.