JK Kuzinduwa Mkakati wa Kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akizungumza jambo kwenye semina hiyo .

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akizungumza jambo kwenye semina hiyo .

Baadhi ya wakuu wa mikoa na waganga wakuu wa mikoa wakiwa katika semina kuhusu kuboresha afya ya uzazi na watoto iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wakuu wa mikoa na waganga wakuu wa mikoa wakiwa katika semina kuhusu kuboresha afya ya uzazi na watoto iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk. Samson Winani akitoa uzoefu wa mkoa wake wa mkakati wa kuounguza vifo vya mama mjamzito na watoto wachanga. Picha na Magreth Kinabo – MAELEZO.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk. Samson Winani akitoa uzoefu wa mkoa wake wa mkakati wa kuounguza vifo vya mama mjamzito na watoto wachanga. Picha na Magreth Kinabo – MAELEZO.

Na Magreth Kinabo – Maelezo

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kwa akinamama na watoto ifikapo mwaka 2015 utakofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Neema Rusibamayila wakati akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya wakuu wa mikoa na waganga wakuu wa mikoa kuhusu kuboresha afya ya uzazi na watoto.

Aidha Dk. Neema alisema uzinduzi huo utaenda sambamba na uzinduzi wa kadi ya ufuatiliaji (scorecard). “Lengo la semina hii ni kuwatambulisha juu ya mpago huu ili kila Mkuu wa mkoa kutathimini maeneo yapi yamefanyiwa vizuri na wapi kuhahitajika msisitizo,” alisema.

 Alisema katika semina hiyo viongozi hao wamepata uzoefu wa wa mkakati wa mkoa Singida na Mara ili kuongeza kasi hiyo kwa siku 500 zilizobakia. Akizungumzia kuhusu upunguzaji wa vifo vya watoto, kwa mujibu wa tathmini ya Umoja wa Mataifa, UN Tanzania imefikia lengo la milenia yaani vifo 54 kwa kila watoto wanaozaliwa 1000, hata hivyo alisema bado jitihada zinahitajika kupunguza zaidi vifo hivyo.

Alisema vifo vya wakina mama kwa sasa ni 454 kwa vizazi hai 100,000. Kwa upande wake, Dk. Ahmad Makuwani kutoka wizara hiyo alisema wakuu wa mikoa na wilaya na timu zao wanawajibu wa kuhakikisha wanapunguza vifo vya uzazi na watoto.

“Wakuu wa mikoa na wilaya mna kazi kubwa ya kuulizia vifo vimetoa kwa sababu gani mkifanya hivyo mtasaidia kupunguza vifo hivo,” alisema Dk. Makuwani. Dk. Makuwani alisema lengo la milinea la kupunguza vifo kwa wakina mama ifikapo mwaka 2015 ni 195 kwa vizazi 100,000.

Akizungumzia kuhusu uzoefu wa Mkoa wa Singida Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dk. Doroth Gwajima alisema ushirikiano wa viongozi, kuzingatia maadili, nidhamu na kila mtu kuwajibika katika nafasi yake itasaidia kupunguza vifo hivyo. Mikoa inayoongoza kuwepo kwa vifo vya wakina mama ni ya Kanda ya Mashariki na Kanda ya Ziwa kwa sababu ya mila na desturi na upatikananji wa huduma karibu na watu.