Kongamano la Uwezeshaji Biashara kwa Nchi Changa za Afrika Lafunguliwa

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda,  akifungua Kongamano la uwezeshaji biashara baada ya mkutano mkuu wa Bali kwa nchi changa  linalofanyika Mkoani Mwanza, kuanzia Mei 16, 2014.

Meza kuu katika Kongamano hilo.

Meza kuu katika Kongamano hilo.

SERIKALI imerudia wito wake kwa sekta binafsi na Wadau wa Maendeleo kuunganisha nguvu zao katika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini na kutumia vyema fursa za kitaifa na kimataifa ili kuinufaisha nchi na wananchi kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Abdallah Kigoda katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo katika Ufunguzi wa kongamano la uwezeshaji biashara baada ya mkutano mkuu wa Bali kwa nchi changa za Afrika.

Waziri Kigoda amesema, Serikali itaendelea kusimamia juhudi zake katika kupunguza gharama za kufanya biashara na kuondoa vikwazo vya kibiashara ili kufanya shughuli hizo kufanyika kwa wepesi, muda mfupi, ufanisi na tija kwa wadau wote.
Amesisitiza kuwa, wakati nchi ikifanya juhudi hizo, ni wakati muafaka sasa kwa nchi zilizoendelea kutimiza makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Bali mwaka 2013 ambapo nchi hizo zilipewa wajibu wa kuzisaidia nchi masiki kifedha, miundo mbinu na teknolojia ili kuzisaidia nchi masikini kupiga hatua.

Viongozi Wakuu katika Kongamano hilo, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mtangamano wa Biashara, Lucas Saronga, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, Profesa Francis Matambalya, Balozi Mstaafu Ali Mchumo na Balozi wa Tanzania- Umoja wa Matafaifa, Modest Mero.

. Picha ya Pamoja ya Wajumbe na Viongozi wakuu wa Kongamano la uwezeshaji biashara baada ya mkutano mkuu wa Bali kwa nchi changa linalofanyika Mkoani Mwanza, kuanzia Mei 16, 2014.

. Picha ya Pamoja ya Wajumbe na Viongozi wakuu wa Kongamano la uwezeshaji biashara baada ya mkutano mkuu wa Bali kwa nchi changa linalofanyika Mkoani Mwanza, kuanzia Mei 16, 2014.

Kwa upande wake Kiongozi wa Waandaaji wa Mkutano huo Profesa Francis Matambalya amesema, Kongamano hili ni fursa muafaka ya kupokea mawazo na uzoefu wa nchi washiriki ili kutoka na msimamo wa pamoja wa kiutekelezaji kuhusu maazimio ya Mkutano wa Bali.

Maeneo yanayopewa umuhimu mkubwa na Kongamano hili ni kukuza uelewa katika mtazamo wa kihistoria, dhana, msingi na hatua mbalimbali ambazo dhana ya Uwezeshaji Biashara imepitia, Hali ya muonekano wa Uwezeshaji Biashara katika Jumuiya za Uchumi Kikanda Afrika na namna bora ya kutumia uzoefu utakaopatikana ili kutengeneza mapendekezo ya agenda kazi ya utekelezaji wa makubaliano ya WTO katika Uwezeshaji Biashara.

Kongamano hili la siku mbili linahudhuriwa na Mabalozi, Viongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara, washiriki kutoka nchi zaidi ya kumi na saba kutoka nchi change za Kiafrika na Wawakilishi wa Taasisi mbali mbali za kitaifa na Kimataifa.