”
Wajumbe wa Link Cities tokea Durban, South Afrika na Marekani wamefika nchini kwa ajili ya kutathmini athari za mabadiliko tabia nchi (climate change). Watakua na ziara katika Manispaa za Kinondoni na Jiji la Tanga.
Picha ya juu kabisa, inaonyesha Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni (mwenye suti, anayeongea mbele), injinia Mussa B. Natty, akiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe hao. Injinia Natty alithibitisha kwamba mabadiliko tabia nchi yameendelea kuathiri Manispaa za Kinondoni kwa njia mbalimbali, ikiwemo mafuriko. Injinia Natty alieleza mkutano huo kwamba mvua zinazoendelea kunyesha zimegharimu maisha ya wakazi 45 wa Manispaa katika maeneo ya Suna bonde la Jangwani, maeneo ya Basihaya.
Baadhi ya sababu zilizotajwa kuchochea athari za mabadiliko tabia nchi ni pamoja na utupaji taka kwenye mifereji ya asili, ambapo asilimia 41 tu ya taka zinazozalishwa hukusanywa na kutupwa kwa siku.
Ujenzi holela, nao umetajwa kama chanzo, ambapo asilimia 70 ya Manispaa ya Kinondoni, ni maeneo yasiyopimwa. Kesho tarehe 13, Wajumbe hao kutoka South Afrika na Marekani watatembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika kwa kiasi kikubwa, ikiwemo maeneo ya mabondeni na ukanda wa bahari.
Picha na Habari na Mdau Maalum wa Thehabari, Dar