KATIKA muendelezo wa kuboresha na kuyapa nguvu maisha ya wateja wake, Kampuni ya vifaa vya umeme Samsung Tanzania ilitangaza kuzindua bidhaa zake mbili mpya Kiyoyozi na jokovu. Magwiji hao wa vifaa vya umeme walianza kwa kuzindua Kiyoyozi kipya chenye muundo wa pembe tatu na muundo wa ubunifu kabisa wenye kusambaza hewa zaidi ambayo inasababisha kutoa baridi zaidi kwenye mazingira ya nyumbani na hata ofisini. Hii ilifwatiwa na jokovu yake ambayo imetengenezwa kwa ajili ya biashara na wateja wa kawaida.
Hafla ambayo ilifanyika Dar es salaam Hoteli ya Serena ilikuwa pia ni jukwaa la mkusanyiko wa mawakala wote wa Samsung jijini. Kwa mtazamo wa mbali wa Samsung kuwa msambazaji wa kwanza mkubwa wa vifaa vya umeme Tanzania, hii ilikuwa ni fursa ya kipekee kukutana na mawakala na wasambazaji wake ambao ndio kiini cha utendaji wao katika soko.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Biashara ya vifaa vya umeme kwa wateja Samsung Bw. Raghu Shetty aliongea kuhusu lengo kuu la kuzindua vifaa hivyo ni uwepo wa mawakala wao akisema kwamba “Ilikuwa ni muhimu kuzindua Friza yetu mpya na kiyoyozi chetu pamoja na mawakala na wasambazaji wetu kwa kuwa ni wahamasishaji wakubwa kwenye jinsi gani bidhaa zetu zinavyofanikiwa katika soko la Tanzania. Hawa ni wakutegemewa na wanawapa wateja wetu uwezo wakupata huduma zetu nyingi zinazokuja na bidhaa zetu”.
Jokovu na Kiyoyozi ni sehemu ya bidhaa za umeme za Samsung ambazo zimetengenezwa kuvumilia mazingira ya kitanzania. Zote zinakuja na sifa tofauti ambazo zinazifanya bidhaa hizo kuendana sambamba na matumizi ya nyumba za kisasa za kitanzania. Bw. Raghu alichangia jinsi gani “Tafiti na muundo vinavyochangia kiasi kikubwa kwa Samsung kuunda bidhaa zao kwa ajili ya soko la kitanzania. Sisi tumeelekeza nguvu katika kuendelea, kuboresha maisha na uzoefu wa wateja wetu”.
Maelezo hayo yalithibitishwa na sifa tofauti za bidhaa. Jokovu kwa upande mmoja inakuja na Stabiliza ambayo inamlinda mteja kutokana na kuharibika kwa jokovu kutokana na hitilafu za umeme. Wakati huo huo ikiendelea kutunza muundo wake na spidi ya kugandisha ambayo ni mara mbili zaidi ya jokovu za kawaida. Na pale ambapo viyoyozi vya kawaida vinachukua muda kueneza baridi katika nyumba za kitanzania, Kiyoyozi chenye muundo wa pembe tatu cha Samsung kimetengenezwa kupooza nyumba haraka, kwa umbali na upana zaidi. Bw. Raghu alimaliza uzinduzi kwa kusema kwamba “Kutokana na sifa tofauti zilizolenga kufikia malengo ya wateja wetu, sisi kama Samsung Tanzania tunamatumaini makubwa na mafanikio ya bidhaa hizi ndani ya soko la kitanzania”.