Gordon Brown Aisifia Tanzani Kielimu Barani Afrika

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete in a bilateral meeting with Rt. Hon. Gordon Brown (MP), UN Special Envoy for Global Education and Former British Prime Minister in the sidelines of the World Economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, May 7, 2014. State House Photos.

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Mr Mark Suzman, President of Global Policy and Advocacy and Country Programmes of the Gates Foundation after holding bilateral talks in the sidelines of the World economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, today May 7, 2014.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa China Mhe. Li Keqiang pembeni ya Mkutano wa Uchumi Duniani kwa bara la Afrika  jijini Abuja, Nigeria, Mei 7, 2014.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa China Mhe. Li Keqiang pembeni ya Mkutano wa Uchumi Duniani kwa bara la Afrika  jijini Abuja, Nigeria, Mei 7, 2014.

MJUMBE Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu ya Kimataifa – UN Special Envoy for Global Education – na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Gordon Brown amesema kuwa Tanzania imefanya vizuri zaidi kuliko nchi nyingine yoyote ya Afrika katika uandikishaji wa watoto kuanza shule.

Aidha, Brown amesema kuwa hana uhakika kama Watanzania wanajua fika kuwa nchi yao imefikia mafanikio makubwa mno ya elimu ambayo bado ni ndoto tu kwa nyingine nyingi za Afrika. Kwa sababu hiyo na kwa sababu ya mafaniko hayo, Brown amesema kuwa Umoja wa Mataifa na taasisi zake na nyingine za kimataifa ziko tayari kuisaidia Tanzania kufikia lengo la kusajili watoto wote kwa asilimia 100 ya watoto wote wanaotakiwa kuingia shule katika muda wa uongozi wa Rais Kikwete na kabla hajaondoka madarakani mwishoni mwa mwaka ujao.

“Mheshimiwa Rais, tunapenda kukupongeza kwa kufanya vizuri sana katika nyanja ya elimu. Haya ni mafanikio ya uongozi wako. Umewezesha asilimia 98 ya watoto wanaotakiwa kuanza shule kuingia shule. Hakuna nchi nyingine ya Afrika ambayo imefikia mafanikio kiasi hiki. Tunapenda kukusaidia na kufanya kazi na wewe ili tufikie asilimia 100, “ amesema Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Uingereza katika mkutano na Rais Kikwete.

Rais Kikwete na Brown wamekutana kwenye Hoteli ya Hilton mjini Abuja ambako wote wawili wanakaa wakati wanahudhuria Kongamano la Uchumi Duniani – kwa Bara la Afrika lilioanza, Mei 7, 2014 katika mji mkuu wa Nigeria. Ameongeza Brown, “Mheshimiwa Rais, sasa tunataka kusaidia kuwapeleka shule kiasi cha watoto 100,000 ambao ni asilimia mbili ambao kwa sasa hawaendi shule.

Tunajua hawa ni watoto wa makabila ya wafugaji ambao wanahamahama kila siku na mifugo yao na watoto wao vile vile. Lakini Serikali yako imepiga hatua kubwa, kubwa kuliko inavyofikiriwa na mataifa mengine ya Afrika katika kukabiliana na hali hiyo.”
Gordon Brown pia amesema kuwa Umoja wa Mataifa na taasisi zake ziko tayari kuisaidia Tanzania katika kuboresha ufundishaji wa masomo ya sayansi ambayo hayana walimu wa kutosha katika Tanzania na duniani pote kwa kutumia njia za ufundishaji za kutumia teknolojia ya habari, mawasiliano na teknolojia.

Rais Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mark Suzman, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani. Aidha, Rais amekutana na kufanya mazunguzo na Bwana Sunnil Bharti Mittal, Mwenyekiti wa Kampuni ya kimataifa ya simu ya Airtel duniani.