RAIA wa Afrika Kusini wanapiga kura kuwachaguwa wabunge, huki pakiwa kuna uwezekano wa chama tawala cha ANC kuendelea kutawa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa toka kwa wapiga kura. Vituo vya kupigia kura ili kutoa fursa kwa raia kutekeleza wajibu wao wa kidemokrasia.
Huu ni uchaguzi wa bunge wa kwanza ambapo vijana walozaliwa baada ya kumalizika utawala wa ubaguzi, watashiriki. Baadhi ya wataalamu wanahisi kwamba shauku na umaarufu uliokuweko wakati wa uhai wa Nelson Mandela kwa chama hicho huenda ukapunguwa, huku wapiga kura wakifikiria zaidi juu ya kuzorota kwa hali ya uchumi na visa vilivyoukumba muhula wa kwanza wa rais Jacob Zuma ikiwa ni pamoja na rushwa miongoni mwa vigogo serikalini.
Raia milioni 25.3 ndiyo watakao piga kura kuchagua wabunge 400 huku wakisubiri tena hapo Mei 21 kupiga kura tena kumchagua rais wa nchi hiyo. Akiwa na umri wa miaka 72 rais Jacob Zuma atagombea nafasi ya urais kwa muhula mwingine wa miaka 5.
Uchaguzi huu umetajwa kuwa wa ‘kutatanisha zaidi’ katika kipindi cha miaka 20 ya nyuma. Mtaalam wa Taasisi ya Utafiti wa Usalama nchini humo, Lizette Lancaster alisema huenda chama cha ANC kikapunguza umaharufu wake katika uchaguzi huo.
Mpinzani mkuu wa chama ANC, Muungano wa Kidemokrasia ‘Democratic alliance’ ulipata kura milioni 16.7 katika uchaguzi wa 2009, licha yakusonga mbele tangu wakati huo, lakini kinazingatiwa kama kituvu chake ni chama cha wazungu.
Changamoto nyingine kwa chama ANC, ni kutoka chama cha ukombozi wa kiuchumi EFF kinacho ongozwa na mkuu wa zamani wa tawi la vijana wa ANC Julius Malema, ambaye alifikia hata kuvaa kofia nyekundu akimuigiza rais wa zamani msosialisti wa Venezuela, hayati Hugo Chaves.
Julius Malema na chama chake kipya katika siasa za afrika kusini aweka mbele utaifa, na kuahidi kutaifa sekta kama benkim na madini na kupokonya mali za wazungu wenye kumiliki mashamba makubwa pasina kulipa fidia, na kugawa upya utajiri wa nchi kwa namna iliyo sawa.
Jana Malema aliwahutubia wachimba migodi waliyo mgomoni tangu januari. katika maeneo ya kakszini. ” Kama hamtopiga kura chama ANC kitasalia madarakani” Hata kama mko mgomoni lazima kesho mwende kupiga kura hata kama mko mgomoni, hatima ya nchi hii iko mikononi mwenu, alisisitiza kiongozi huyo kijana “.
Hadi kwenye saa za mwisho jana viongozi wa usalama walikuwa wakitowa mwito ya utulivu kwenye siku hii ya uchaguzi, wakati maandamano yenye ghasia yalivikumba vitongoji na mitaa inayo kaliwa na watu wengi masikini hususan Johannesburg.
Afrika kusini imesalia nchi isiyo na usawa licha ya kumalizika utawala wa ubaguzi, ambapo wazungu waanapokea mara 6 zaidi ya raia weusi. Pia hawakabiliwi na ukosefu ajira kama ilivyo kwa weusi na wakipata elimu ambayo weusi hawaipati. Ikiwa na ukuwaji unao kadiriwa sawa na asilimia 3, 3 katika miaka 20 ya nyuma Afrika kusini bado iko mbali na kutimiza mkakati wa kuwapatia ajira mamilioni ya raia wake wasio na kazi.
-DW