Diamond Kiboko, Ambadili Jina Wema Sepetu…!

Diamond na Wema wakibusiana kwa ishara ya upendo.

Diamond na Wema wakibusiana kwa ishara ya upendo.

Na Mwandishi Wetu, dev.kisakuzi.com Dar

MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya anayeendelea kukubalika katika tasnia hiyo, Naseeb Abdul au maarufu kwa jina la Diamond Platinum sasa amembadili jina mpenzi wake waliyerudiana hivi karibuni msanii wa kuigiza filamu, Wema Sepetu.

Diamond alijikuta akimbadili jina mpenzi wake bila kutegemea baada ya juzi usiku kujishindia tuzo saba katika vipengele tofauti alivyoshindanishwa kwenye Shindano la Tuzo za Muziki, maarufu kama ‘Kilimanjaro Tanzania Music Award’ (KTMA).

Baada ya tukio hilo la ushindi wa tuzo, Wema Sepetu mpenzi wa Diamond sasa amebatizwa jina na kuitwa MRS MI-AWARDS jina alilopewa na staa mwenzake wa filamu, Elizabeth Michael a.k.a Lulu baada ya mpeziwe kutwaa tuzo kibao.

Lulu alimpa jina hilo Wema baada ya kuandika kwenye mtandao kuwa anapenda ambadili jina Wema na kuitwa Mrs Mi-Awards kuanzia sasa. “Naomba kuanzia leo nikiite MRS MI AWARDS kha…!!! tuachane na jina jipya bi dada…!,” aliandika Lulu kwenye ukurasa wake wa instagram juzi.

Diamond alishinda tuzo zote saba alizoshindanishwa na kuweka historia katika shindano la KTMA. Tuzo saba alizonyakuwa Diamond juzi ni ya Wimbo Bora wa Pop, Mwimbaji Bora wa Kiume wa Kizazi Kipya, Msanii Bora wa Kushirikishwa/Kushirikiana, Mtunzi Bora wa Mwaka wa Kikazi Kipya, Video Bora ya Mwaka, Wimbo Bora wa Mwaka na Mtumbuizaji Bora wa Kiume.Katika vipengele hivyo Diamond alifanikiwa kutwaa tuzo zote saba na kuwabwaga washindani wake.

Katika hafla hiyo moja ya tuzo hizo alikabidhiwa na mpenzi wake, Wema Sepetu ambaye alionekana kufuraishwa zaidi na mafanikio ya rafiki yake huyo ambaye amerudiana kimapenzi hivi karibuni na kuonesha mapenzi motomoto.