Matukio Tamasha la Pasaka Mkoani Shinyanga

Faraja Ntaboba mwimbaji wa muziki wa injili kutoka Congo DRC akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Faraja Ntaboba mwimbaji wa muziki wa injili kutoka Congo DRC akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

1

Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa Tamasha la Pasaka lililofanyika mkoani humo likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili, Tamasha hilo limeandaliwa na kampuni ya Msama Promotion na linaendelea Kesho kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambapo Mwanamuziki maarufu wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Rebecca Malope atafanya mambo mamkubwa

jijini Mwanza. 

 2

Kundi la wanenguaji wa mwimbaji Rose Muhando wakifanya vitu vyao kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga leo.

3

Mwimbaji Rose Muhando akicheza na watoto wakati alipokuwa akiimba katika Tamasha la Pasaka mjini Shinyanga.

4

Mwimbaji wa muziki wa injili Upendo Kilahiro akiimba jukwaani huku akipigwa tafu na waimbaji wenzake wa muziki wa injili kutoka kushoto ni Grace Mwikwabe, Tumaini Njole, Faraja Ntaboba kuoka nchini Congo DRC na Mess Chengula.

5

Mwimbaji Upendo Nkone wa pili kutoka kulia akicheza na waimbaji Faraja Ntaboba kulia na wenzake Grace Mwikwabe kushoto na Tumaini njole wakati alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani

7

Faraja Ntaboba mwimbaji wa muziki wa injili kutoka Congo DRC akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. 8

Mwimbaji Mess Chengula naye alifanya mambo makubwa katika tamasha hilo. 9

Mess Chengula akionyesha uwezo wa ktawala jukwaa katika tamasha hilo. 10

Mwimbaji Grace Mwikwabe akifanya vitu vyake ambapo kesho  anatarajiwa kuzindua albam yake kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

11

Mwimbaji Tumaini Njole amefanya mambo makubwa pia. 12

Mashabiki wa muziki wa injili waliohudhuria katika tamasha hilo wakipata burudani kutoka kwa waimbaji mbalimbali katika tamasha hilo.

Picha na FullShangwe Blog Shinyanga.