Viatu Virefu Vyamuumbua Msanii Vanesa Mdee Jukwaani…!

Msanii Vanessa Mdee (Picha na Bongo5)

Msanii Vanessa Mdee (Picha na Bongo5)

Na Mwandishi Wetu, Dar

UVAAJI wa viatu virefu bila kuwa na uzoefu navyo au kufanya mazoezi namna ya kuvitembelea usiku huu vilimuumbua msanii maarufu wa bongo fleva, Vanesa Mdee katika Ukumbi wa Mlimani City. Tukio hilo lilimkumba msanii Mdee akiwa katika jukwaa la Kilimanjaro Tanzania Music Award (KTMA) alipopanda kuchukua tuzo yake ya Mwanamuziki Bora wa R&B 2014.

Msanii huyo akiwa jukwaani kukabidhiwa tuzo hiyo akizunguka zunguka viatu vilimtegua na nusura ale mweleka akiwa jukaani lakini aliwahi kujizuia na kuwaacha watu waliokuwa wakimshuhudia wakiduwaa.
Vanesa Mdee alipanda jukwaani akiwa amevaa viatu virefu maarufu kama mchuchumio ambavyo vilionekana kumsumbua na kumnyika uhuru kabla ya kutaka kumuangusha. Baadhi ya mashuhuda walianza kunong’ona kwa kuwalaumu baadhi ya kina akiwemo Mdee kwa kuvaa viatu ama mavazi ambayo yamekuwa yakionekana kumnyima uhuru katika matembezi.

Hata hivyo, ili kuvunja soo Vanesa Mdee aliamua kupanda tena kwa mara ya pili jukwaani akiwa na viatu hivyo na kuimba navyo lakini safari hii alijitahidi kuvitumia hivyo havikutaka kumbwaga tena na kumuaibisha jukwaani. Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music (KTMA) zinafanyika usiku huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.