Matukio Picha Tamasha la Pasaka Jijini Dar es Salaam

 Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na kwa mbwembwe wakati alipokuwa akifanya vitu vyake  kwenye uwanja wa Taifa jana.

Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse
Phoofolo akicheza kwa mbwembwe wakati alipokuwa akifanya vitu
vyake kwenye uwanja wa Taifa katika Tamasha la Pasaka lililofanyika jana.

 Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Tamasha la Pasaka akizungumza na mashabiki mbalimbali waliojitokeza katika tamasha hilo, ambapo aliwaomba kuwa watulivu wakati huu wa mchakato wa Katiba Mpya, Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama na katikati ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki.
 Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na mashabiki wake wakati alipokuwa akifanya vitu vyake  kwenye uwanja wa Taifa jana.
 Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti akiimba jukwaani jana.
  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa, Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete akiongozwa kuelekea jukwaani na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama
 Mwimbaji wa ijini kutoka nchini Uingereza Dayo Bello akiimba na mkewe Ruth Tobi wakati wa tamasha la pakasa kwenye uwanja wa Taifa jana.
 Mwimbaji Jesca BM naye alipagawisha mashabiki
 Mchungaji mtarajiwa Masanja Mkandamizaji akifanya vitu vyake jukwaani
 Umati uliojitokeza  katika tamasha hilo.
 Upendo Kilahiro akiimba jukwaani na kundi la Victoria Singers.
 Mashabiki mbalimbali wakimshuhudia mwanamuziki Kekeletse Phoofolo hayupo ichani wakati alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani.
Ikafika zamu ya Upendo Nkone
Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse
Phoofolo kazi moja tu burudani .
Rose Muhando na kundi lake wakipagawisha kwenye tamasha la Pasaka jana katika uwanja wa Taifa.
(Picha na FullShangwe Blog)