Juma lililopita tuliangalia masuala matanohttp://www.thehabari.com/habari-tanzania/kama-una-mpango-wa-kuoa-siku-moja-lazima-usome-hii , ambayo unatakiwa uzingatie kabla haujafanya maamuzi mazito ya kufunga ndoa na mpenzi wako. Leo tunaendelea na masuala matano ya mwisho, na kwa ujumla yake yanakuwa kumi.
6. Je wewe na mpenzi wako mnachangia dini? Kama mpo dini tofauti au hata madhehebu tofauti, basi ni kitu cha kuwa makini sana. Hili ni suala zito, kwasababu mkija kuwa na watoto huko mbele ya safari wataenda kuabudu wapi? Je kwenye kanisa (au msikiti) lako au la mpenzi wako? Majibu ya maswali haya yanaweza yakaleta mgogoro mkubwa, mtaalam anatahadharisha.
7. Je mnakubaliana ni namna gani watoto walelewe? Kama kila mmoja wanu ana imani zake na mikakati linapokuja suala la kulea watoto, basi ndoa yenu itakuja kuwa na matatizo. Kwa mfano, kama wewe una amini kumkaripia mtoto inatosha na mwenzio ana amini kwamba karipio bila mikwaju mtoto hajalelewa basi mtakuwa mnagombana kila siku linapokuwa suala la “kumdisplini” mtoto.
8. Je wewe na mpenzi wako mnapenda kushiriki kwenye michezo au viburudisho vinavyofanana (fun activities)? Mtaalam anasema kwamba kama mnatofautiana hobi kadhaa sio mbaya, lakini kama tofauti ni kubwa sana, basi mtakuja kuchokana mapema, na pengine sio suala jema kufunga ndoa. Hakikisheni mnazo hobi za kufanana za kutosha!
9. Kama wewe na mpenzi wako mnatofautiana kuhusu mahala pakuishi, basi sio suala jema kufunga ndoa, kwani hamto kuwa watu wenye furaha katika ndoa yenu, mtaalam anasema. Kama mpenzi wako anapenda kuishi Dar na wewe unapenda kuishi Arusha (au hata nchi tofauti), basi ikibidi muishi Dar, mmoja wenu atakuwa hana raha na huo ni mwanzo wa malumbano.
10. Je wewe na mpenzi wako mnatengeneza pesa za kutosha kwa ajili ya kujikimu kila mwezi? Mtaalam anasema hili ndio suala muhimu kuliko yote, kwani kama ni watu wa kukopakopa kila mwezi, itakuwa majanga zaidi mkija kuoana!
Je unafikiri haya ni masuala ya msingi kuzingatia kabla haujafanya maaamuzi ya kufunga ndoa? Tupe maoni yako………………..
Imetayarishwa na: Thehabari.com
Source: Yahoo Voices