Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa Wilaya ya Bahi tarehe 14.4.2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akiwapungia wanafunzi na wananchi wa Bahi waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa saratani ya shingo ya kizazi mjini hapo tarehe 14.4.2014.
Uzinduzi wa Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa Macho wa Mkoa wa Dodoma Dk. Frank Magupa, wakati alipotembelea maonesho ya kitabibu yaliyofanyika sambamba na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa wilayani Bahi tarehe 14.4.2014.
Mamia ya wananchi wa Bahi wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na viongozi wa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi iliyofanyika huko Bahi, Mkoani Dodoma tarehe 14.4.2014.
Tanzania
(TBC1) Bwana Hamis Mwege kwa kazi kubwa ya kuelimisha umma kuhusu kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake hapa nchini. Vyombo vingine vilivyopata cheti ni Channel Ten na ITV.” src=”http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/04/IMG_1018.jpg” width=”640″ height=”426″ /> Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC1) Bwana Hamis Mwege kwa kazi kubwa ya kuelimisha umma kuhusu kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake hapa nchini. Vyombo vingine vilivyopata cheti ni Channel Ten na ITV.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha vifaa mbalimbali vinavyotumika na madaktari wakati wa kuwapima wanawake ili kufahamu kama wana maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo wilayani Bahi tarehe 14.4.2014.
Picha na John Lukuwi