Rais Kikwete Aipongeza Timu ya Watoto wa Mitaa, Yatambulishwa Bungeni…!

Mfugaji bora wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC), Frank William na Kapteni Msaidizi Emmanule Amos akipeana mkono na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba.

Mfugaji bora wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC), Frank William na Kapteni Msaidizi Emmanule Amos akipeana mkono na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba.


Picha ya kumbukumbu na timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania.

Picha ya kumbukumbu na timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania.

RAIS Jakaya Kikwete ameipongeza Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kwa kutwaa Kombe la Dunia huko Rio de Janeiro – Brazil. “Mmetuwakilisha vyema, ninawapongeza sana, pia mmewapa moyo watoto wengine wote wenye vipaji maalum lakini hawakubahatika kuwa na makazi rasmi, hongereni sana” Rais amesema.

Timu hiyo ya watoto wenye umri chini ya miaka 16 (under 16) ilipangwa kundi la 2 ambapo wamekuwemo na Nchi za Argentina, Nicaragua, Philippines na Burundi na kulikuwa na makundi matatu. Tanzania iliingia nusu fainali kwa kuwa mshindi wa pili na pia kuminyana na Marekani na kuichapa mabao 6-1 na baadae kuitoa Burundi kwa mabao 3-1.

“Hongereni kwa kujituma na kucheza kwa ustadi”. Rais amesema na kuwaasa watoto “ongezeni bidii, nidhamu na mazoezi ya kutosha na hakika mtafanikiwa zaidi na kulibeba jina la Tanzania mbali zaidi ya hapa katika ulimwengu wa soka duniani, kwani hakuna kisichowezekana kama mtazingatia maelekezo, mafunzo, bidii na nidhamu ya yote mnayofanya” Ameongeza.

TIMU YA WATOTO WA MITAANI YATAMBULISHWA BUNGENI
Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania iliyotwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani nchini Brazil baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 kwenye fainali imetambulishwa leo (Aprili 11 mwaka huu) katika Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.

Baadaye timu hiyo leo itapata chakula cha mchana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda. Saa 10 jioni itatembeza kombe hilo katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma katika gari za wazi.

Jioni imeandaliwa hafla maalumu ya chakula pamoja na burudani hapo hapo mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.

CHACHA KUCHEZESHA MICHUANO YA AYG
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua mwamuzi msaidizi wa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ferdinand Chacha ameteuliwa kuchezesha michezo ya Vijana ya Afrika (AYG- African Youth Games).

Michezo hiyo ya kwanza ya Afrika itachezesha jijini Gaborone, Botswana kuanzia Mei 22-31 mwaka huu. Tanzania pia itashiriki katika mashindano hayo ya vijana wenye umri chini ya miaka 15.

Mechi ya raundi ya 25 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ashanti United inachezwa Jumapili (Aprili 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Na si Jumamosi (Aprili 12 mwaka huu) kama taarifa yetu ya awali ilivyosema. Mechi nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya) wakati Coastal Union itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Keshokutwa (Aprili 13 mwaka huu) kutakuwa na mechi nyingine nne za kukamilisha raundi hiyo. Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Yanga.

Mtibwa Sugar itacheza na Ruvu Shooting (Uwanja wa Manungu, Morogoro), Mgambo Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.