Kama Una Mpango Wa Kuoa Au Kuolewa, Lazima Usome Hii!

Perfectly Beautiful African American Couple

 

 

Je umeshawahi kuwa na mashaka yeyote kuhusu kuoa? Je unafikiri haupo tayari kuoa? Kama majibu ya maswali haya ni NDIO, basi zingatia masuala yafuatayo, ambayo yatakusaidia kutambua kama upo tayari kuoa au kama mazingira ya kuoa ni salama kwako. Michele K, mtaalamu wa masuala ya mapenzi na mahusiano, ambaye ameandika na kuuza maandiko (Articles) zaidi ya 550, anasema uzingatiaji wa masuala haya muhimu, kutakusaidia kujiepusha na majuto baadae. Zaidi, uzingatiaji wa masuala haya kutakusaidia kujiepusha na upotevu mkubwa wa pesa na muda. Masuala yenyewe ni kama ifuatavyo:

  1. Kama wewe na mpenzi wako (mwanamke au mwanaume unayetoka nae) mpo kwenye madeni makubwa ya pesa, basi sio “good idea” kufunga ndoa. Hii ni dalili kwamba ndoa yenu itakuja anza vibaya, kwa nyinyi kutumia muda mwingi kugombana kuhusu pesa na madeni.
  2. Je wewe au mwenzako ana mtoto katika ndoa au amahusiano ya zamani? Kama kuna mtoto, basi lazima uzingatie ugumu utakao jitokeza pindi mtakapo funga ndoa na kujaribu kuziunganisha hizi familia mbili. Mtaalamu anasema kwamba watoto wa kambo mara nyingi huleta matatizo kwa wazazi wao wa kambo kutokana na masuala ya tabia. Ukiachalia masuala ya tabia za mtoto/watoto, kuna suala la mtoto husika kuwa bado na hasira kwanini wazazi wake wa kumzaa hawapo pamoja. Hii inaweza ikamfanya mtoto awe kichwa ngumu na kukuletea wewe mzazi wa kambo matatizo!
  3. Je unao uwezo wa kudili na Ex (mpenzi wa zamani) wa mpenzi wako? Kama hauna ubavu, basi bora ukatae ndoa, maana ukishafunga ndoa, utalazimika kwa njia moja au nyingine kudili na ma Ex, ambao wengi wao ni wakorofi na hawaishi visa. Kama mpenzi wako ana mtoto/watoto na mpenzi wake wa zamani, basi suala ndio linazidi kuwa ‘complicated’. Mpenzi wa zamani anaweza akawa ana tumia watoto kuvuruga hiyo ndoa yenu. Kama mazingira yapo hivyo, usioe au kuolewa, mtaalamu anashauri.
  4. Kama haufurahii tabia za mpenzi wako sasa hivi, basi usifikiri kwamba mkija kuoana eti ndio wakati wa kubadilishana tabia. Kama kuna tabia zozote hauzipendi, basi huyo mpenzi wako hana sifa za kuwa mke wako au mume wako. Masuala ya kutaka kubadilishana tabia wakati wa ndoa huleta ugomvi mkubwa na hatimaye ndoa husika kuvunjika. Hakikisha umempenda mpenzi wako kama alivyo na tabia zake zote kabla haujafunga ndoa, vinginevyo ndoa yako itaishia kuvunjika tu! Mtaalamu anatoa onyo!
  5. Kama wewe na mpenzi wako hamna malengo yanayofanana (same goals), basi hiyo ndoa mnayofikiria kufunga tayari ipo matatani. Unatakiwa wewe na mpenzi wako muwe katika malengo yanayofanana, ili kuweza kuifurahia ndoa yenu. Wapenzi wenye malengo ya kimaisha tofauti, huishia kuchokana mapema, na ndoa huvunjika!

Tukutane Juma lijalo kwa masuala matano yaliyobaki……………………..

 

Imeandaliwa na: Thehabari.com

 

 

Source: Yahoo Voices