Nyangwine Kuwashtaki Makada Wanaomuhujumu kwa Kinana

Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao chake na Kamati ya Siasa ya mkoa wa Kigoma, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya mkoa huo, jana, Aprili 9, 2014. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume na kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Dk. Walid Kaborou.

Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao chake na Kamati ya Siasa ya mkoa wa Kigoma, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya mkoa huo, jana, Aprili 9, 2014. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume na kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Dk. Walid Kaborou.

VURUGU na kampeni chafu zinazofanywa na baadhi ya makada wa CCM wanaojipanga kuwania ubunge katika jimbo la Tarime, zimechukua sura mpya.

Hatua hiyo imetokana na mbunge wa jimbo hilo Nyambari Nyangwine (pichani), kuweka bayana kuwa atawasilisha malalamiko kwa uongozi wa CCM ngazi ya wilaya, mkoa na taifa.

Juzi, baadhi ya wanachama wa CCM wilayani Tarime, walilalamikia kampeni chafu  zinazofanywa na baadhi makada na kusababisha makundi ambayo ni hatari kwa Chama.

Hata hivyo, baadhi ya makada hao ambao baadhi wametajwa kuungwa mkono na baadhi ya viongozi wa CCM wilayani humo, wamekuwa wakieneza siasa chafu za ukabila, jambo ambalo limeelezwa kuwa ni hatari.

Makada hao ambao baadhi walishindwa kwenye kura za maoni, ambapo sasa wameanza kujipanga upya lakini wakitumia njia ambazo ni kinyume na taratibu za CCM.

Taarifa ya Nyangwine kwa vyombo vya habari jana, imesema kuwa atawasilisha malalamiko yake ikiwa ni pamoja na kuwataja kwa majina makada hao.

Imesema kuwa makada hao wamekuwa wakieneza siasa za chuki zenye lengo la kukwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Hata hivyo, alisema kamwe hatishwi na makada hao kwa kuwa baadhi waligombea mara kadhaa na kushindwa hivyo jimbo hilo kutawaliwa na wapinzani kwa miaka 10.

Alisema CCM ni chama chenye demokrasia na kinajali haki za kila mwanachama katika kuwania uongozi, lakini kina taratibu zake ambazo ni lazima zifuatwe ikiwa ni pamoja na kusbiri muda mwafaka wa kufanya kampeni na si kuwahujumu waliopo madarakani.

“Nitawasilisha malalamiko yangu rasmi kwa uongozi wa chama ngazi zote hadi kwa Katibu Mkuu wetu (Abdulrahaman Kinana), sasa hivi ni wakati wa kutekeleza Ilani za Chama kwa wananchi si kufanya kampeni ili kukwamisha kazi.

“Waniache nitumikie wananchi walionichagua na muda ukifika waje tupambane kwa hoja ndani ya Chama, haya wanayoyafanya sasa hivi ni uhuni na kutaka kurejesha makundi ambayo mwisho wa siku yatakigharimu chama chetu.

“Baadhi ya wanaoendesha siasa hizi chafu ni wanasiasa ambao wameishiwa sera na goigoi na ndio sababu wameshindwa mara kadhaa kwenye uchaguzi,” alisema Nyangwine kwenye taarifa yake.