WAKATI mpinzani wa Bondia Francis Cheka, Gavad Zohrevand, anawasili nchini kesho, mpinzani wa Francis Miyeyusho, Agelito Merin, atawasili kesho kwa ajili ya pambano lao litalaofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Mratibu wa pambano hilo, Mussa Kova, alisema kuwa bondia huyo atawasili majira ya saa 9, alasiri, kwa kutumia ndege ya Emirates, akitokea nchini Iran. Kova alisema Merin, ambaye ni mpinzani wa Miyeyusho atawasili saa moja asubuhi kwa ndege ya Qatar. Alisema kila kitu kipo vizuri ambapo mabondia hao tayari wameshatumia tiketi zao za kuja nchini, kwa ajili ya pambano hayo.
“Kila kitu kinaendelea vizuri ambapo wapinzani wao wote wapo njia, ambapo mpinzani wa Cheka atawasili Jumatano na wa Miyeyusho atawasili siku ya Alhamis,” alisema Kova.
Pia Kova alisema licha ya kuwepo na mapambano hayo kuwakuwa na mapambano mengine mawili ya utangulizi. Kova alisema moja ya pambano litakuwa kati ya Cosmas Cheka na Ibrahim Clasic, ambapo pambano hilo litakuwa la ubingwa wa Taifa, litakuwa la raundi 10. Pambano la Miyeyusho ambalo litakuwa na ubingwa wa Dunia wa WBU lintakuwa la raundi 12, wakati la Cheka litakuwa na Kirafiki la Kimataifa litakuwa la raundi 8.