Ndugu zangu,
Leo Jumatatu, Aprili 7, Redio yako ya Kijamii ya KwanzaJamii imeandika historia kwa kuwa redio ya kwanza hapa nchini kuwaletea wasikilizaji dondoo za habari za magazetini kutokea kwenye soko lenyewe la habari, niĀ pale kona ya Uhuru na Msimbazi, Kariakoo.
Ni kipindi cha kila siku kuanzia saa kumi na moja na nusu alfajiri. Mwandishi/ Mtangazaji wa KwanzaJamii atakuwa sokoni hapo na kuungana moja kwa moja na studio za Kwanzajamii radio Iringa. Sambamba na redio, habari hizo na picha za magazeti yenyewe zitarushwa pia kwenye Mjengwablog.com. Ikumbukwe, Mjengwablog ilikuwa ni blogu ya kwanza hapa nchini kuanza kurusha kwenye blogu dondoo za magazetini. Usikose kufuatilia na kuzipata habari zikiwa motomoto kutoka Soko la habari Kariakoo…http://www.mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/10489-kutoka-soko-la-habari-kariakoo.html#.U0JH6ldQ7U4