Sitta Awapoza ‘Wapinzani’ Bunge la Katiba…! Bunge la Katiba Laendelea

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba John Mnyika akichangia azimio la kufanyia marekebisho ya kanuni za Bunge Maalum leo mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba John Mnyika akichangia azimio la kufanyia marekebisho ya kanuni za Bunge Maalum leo mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kushoto) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma na Mjumbe wa Bunge hilo Salehe Pamba (kulia).

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa
(kushoto) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma na Mjumbe wa Bunge hilo Salehe Pamba
(kulia).

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Moses Machali akichangia azimio la kufanyia marekebisho ya kanuni za Bunge Maalum leo mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Moses Machali akichangia azimio la kufanyia marekebisho ya kanuni za Bunge Maalum leo mjini Dodoma.

Na Magreth Kinabo- Dodoma

MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta ametangaza rasmi majina mengine ya ziada ya wajumbe wapya wa Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo. Majina hayo yametangazwa leo na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Hassan Suluhu mjini Dodoma kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bunge hilo.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba Sitta amefanya uteuzi huo, ili kuleta muafaka kwa kushirikisha wadau kutoka uwakilishi wa upinzani, ambao hawakuweza kuchaguliwa kwenye kamati 12 za Bunge  hilo.

Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo aliyataja majina hayo ya walioteuliwa kuwa ni pamoja na Freeman Mbowe, Abubakar Khamis Bakari, Fatma Abdulhabib Fereji, Nakazael Lukio Tenga na Amon Mpanju.