Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba nne ya Bunge Maalum la Katiba, Dk. Sira Ubwa Mamboya (kushoto) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta (kulia) alipoitembelea Kamati hiyo jana mjini Dodoma kujionea kazi inayoendelea ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya. Mwingine ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Christopher Ole Sendeka (katikati).
Mjumbe wa Kamati namba nne ya Bunge Maalum la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila akiuliza swali wakati Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta (hayupo pichani) alipoitembelea Kamati hiyo mjini Dodoma kwa ajili kujionea kazi ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya. Picha zote na Kamati ya Bunge Maalum la Katiba (BMK).
Mjumbe wa Kamati namba nne ya Bunge Maalum la Katiba, Dk. Terezya Huvisa akiuliza swali wakati Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta (hayupo pichani) alipoitembelea Kamati hiyo jana mjini Dodoma kwa ajili kujionea kazi ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Kamati namba kumi na mbili ya Bunge Maalum la Katiba Goodluck Ole – Medeye akichangia mjini Dodoma wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alipoitembelea Kamati hiyo kujionea kazi inayoendelea ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya.