TGNP Mtandao Wafunga Warsha ya Siku 3 kwa Waandishi wa Habari Shinyanga

Kaimu meneja wa habari na mawasiliano kutoka TGNP Mtandao bi Kenny Ngomuo Kaimu meneja wa habari na mawasiliano kutoka TGNP Mtandao bi Kenny Ngomuo  akizungumza leo katika ukumbi wa papa Paulo wa pili Ngokolo mjini Shinyanga wakati katika siku ya mwisho ya warsha ya siku tatu kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ambayo imeanza tarehe 27,2014 ikiwa na lengo la kupanua uelewa kuhusu harakati za ukombozi wa wanawake katika muktadha wa mjadala wa madai ya wanawake katika katiba mpya,kupata mrejesho wa masuala  yaliyojiri katika warsa  ya wandishi  wa habari  mwaka 2013,kujadili masuala makuu yaliyojiri katika uragabishi uliofanywa na TGNP Mtandao  mwaka huu katika kata ya Mondo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga pamoja na kutafakari kwa pamoja wajibu wa waandishi wa habari katika kuandika habari za mchakato wa katiba na ushiriki  katika uchaguzi wa serikali za mitaa sambamba na kuweka mipango baada ya warsha hiyo.

Sam Bahari mwandishiAnayezungumza ni bwana Sam Bahari mwandishi wa habari gazeti la Mtanzania/Rai/The African akichangia mawili matatu katika warsha hiyo ikiwemo kusisitiza suala la kuboresha daftari la wapiga kura ili kumpa fursa kila Mtanzania kushiriki kikamilifu katika zoezi la upigaji kura.Lakini pia akazungumzia changamoto mbalimbali wanazokabiliana waandishi wa habari wakati wa uchaguzi ikiwemo kukosa usafiri hali inayochangia watumie magari ya viongozi wa vyama vya siasa

Anna Sangai ambaye ni afisa kutoka TGNP MtandaoAnna Sangai ambaye ni afisa kutoka TGNP Mtandao anayehusika na masuala ya utafiti,ushawishi na ujenzi wa nguvu za pamoja akizungumza katika warsha hiyo ya siku kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia zoezi la uraghabishi lililofanywa na TGNP Mtandao katika kata ya Mondo wilayani Kishapu kwa muda wa wiki mbili kuanzia tarehe 11,Machi,2014,ambapo walikutana na wananchi wa vijiji mbalimbali kama vile Buchambi,Buganika,Mwabayanda na Mwigumbi.Alisema katika zoezi hilo wananchi wa kata hiyo waliibua mambo sita wanayokabiliana nayo kama vile tatizo la maji ambapo wanawake wanatumia muda mwingi kufuata huduma ya maji na huko wanakumbana na changamoto nyingi ikiwepo kubakwa.Tatizo jingine lilionekana katika sekta ya afya ambao vifaa tiba,huduma za maji,lugha mbaya kwa watoa huduma,ukosefu wa vyoo katika vituo na zahanati,wanawake kulipishwa shilingi elfu 10 ya kujifungulia n.k.Tatizo jingine lililoibuliwa na wananchi ni katika sekta ya elimu kama vile walimu kutumikisha wanafunzi na wengine kuwataka kimapenzi.Jambo jingine ni kuhusu ardhi na uwekezaji,ukatili wa kijinsia pamoja na uongozi na uwajibikaji

Kaimu meneja wa habari na mawasiliano kutoka TGNP Mtandao bi Kenny Ngomuo Kaimu meneja wa habari na mawasiliano kutoka TGNP Mtandao bi Kenny Ngomuo akifunga warsha hiyo ambapo aliwashukuru waandishi wa habari kwa kushiriki kikamilifu katika warsha hiyo kwa michango yao na kwamba TGNP Mtandao imejifunza mengi kutoka kwao huku akiwasisitiza waandishi wa habari kutimiza wajibu wao na kufuata maadili ya kazi yao,lakini pia kuandika habari zinazozingatia usawa wa kijinsia

picha ya pamojaPicha ya pamoja washiriki na maafisa kutoka TGNP baada ya warsha hiyo kuisha mjini Shinyanga