Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani muda mfupi kabla ya kufanya mazungumzo ya faragha (tete-a-tete ) huko Ikulu tarehe 25.03.2014.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dk. Frank-Walter Steinmeier na baadhi ya viongozi aliofuatana nao wakati walipomtembelea Rais Dk. Kikwete huko Ikulu tarehe 25.3.2014.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe wakipiga picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mheshimiwa Dk. Frank-Walter Steinmeier na ujumbe aliofuatana nao wakati wakipomtembelea Rais Dk. Kikwete huko Ikulu tarehe 25.3.2014.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Dk. Frank- Walter Steinmeier wakitoka nje kwenda kuona sehemu ya jengo la ikulu lililojengwa na Wajerumani wakati wakiitawala Tanganyika. Wengine waliofuatana nao ni Balozi wa Tanzania huko Ujerumani, Phillip Marmon na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Dorah Msechu.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonyesha wageni wake jengo la ikulu sehemu iliyojengwa na Wajerumani (jengo halionekani pichani) mara baada ya kufanya mazungumzo na ugeni huo. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI.