Rais Kenyatta Awataka Wana EAC Kutoa Kipaumbele Masuala ya Usalama

Rais Uhuru Kenyetta wa Kenya.

Rais Uhuru Kenyetta wa Kenya.


Na Ronald Ndungi, EANA, Arusha

RAIS Uhuru Kenyetta wa Kenya, amezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutoa kipaumbele katika mtangamano wao kwenye sekta ya ulinzi na usalama. Akifungua kikao cha 22 cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA) mjini hapa Jumanne, Rais huyo alisema kwamba ugaidi bado ni tishio kubwa kwa jumuiya hiyo.
 
“Hatua yoyote ya nchi moja pekee ya kukabiliana na tatizo hili la kiusalama haitoshi kwani zinahitajika zaidi juhudi za pamoja,” alisema Kenyatta.
 
Alibainisha kwamba kanda hiyo imeshatia saini makubaliano ya usalama ambayo anatarajia yataanza kufanyakazi kabla ya mwisho wa mwaka huu. Kenyatta pia alishutumu matukio ya hivi karibu ya kuongezeka kwa biashara haramu ya mazao ya wanyamapori hususani ni pembe za ndovu na faru licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na kanda hiyo kupambana na ujangili.
 
“Kwa bahati mbaya Afrika Mashariki imetambuliwa kuwa ndiyo chanzo kikuu na njia inayotumika zaidi katika biashara hii haramu,” alisema.
 
“Katika kipindi kati ya Januari na Oktoba, 2013 pekee, zaidi ya tani 10 za pembe zilikakamatwa katika bandari ya Mombasa,” alisema. Tanzania naye imekuwa ikikabiliowa na hali kama hiyo kwa miezi ya hivi karibuni.
 
Kiongonzi huo alisema matukio hayo siyo tu yanatishia manufaa yanayopatikana moja kwa moja kwa maisha ya jamii katika maeneo hayo lakini pia ni tishio kwa sekta ya utalii ambayo baadhi ya nchi wananchama za EAC inachangia zaidi ya asilimia 10 ya mapato ya nchi kwa mwaka.
 
“Kinachotisha zaidi ni wasiwasi wa jumla kwamba mapato haramu yanayotokana na biashara hii inawezekana kuwa ndiyo inayofadhili shughuli za kitalii,” alionya.