Leo ni Leo, Je Manchester United Wataweza Kulipiza Kisasi?

kompany-vincent-wayne-rooney-manchester-united-city-premier-league_3008313

Manchester City wananafasi ya kuonyesha kuwa wanastahili kuutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza na kuziba nafasi iliyopo kati yao na Chelsea.

Manchester United walichapwa 4-1 ndani ya Etihad stadium hapo mwezi wa tisa mwaka jana wakati ambapo David Moyes ndio alikuwa anaanza anza kuifundisha Man United, na presha imekuwa ikiongezeka kila siku kwa miezi sita iliyopita.

Mpaka sasa zimebaki game 8 mpaka kufikia mwisho wa ligi kwa muhula huu, Manchester United, inavyoonekana hawawezi kuingia katika timu kuu nne.

Man united wapo nafasi ya 7 kwa sasa, point 11 nyumba na Arsenal ambao ndio wanasimama katika nafasi ya nne.

usikose kuangalia mechi hii ya kusisimua, na baada ya game rudi hapa dev.kisakuzi.com kuangalia matokea ya timu nyingine pamoja na maoni ya wahariri na wasomaji wetu.