Katibu wa NEC CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza baada ya kuzindua tawi la wanachama wa CCM la wasomi wa Chuo Kikuu cha Tumaini (SIMCO), katika mkutano uliofanyika katika mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro, jana. Wengine kutoka kushoto, wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo Swaijaro na kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kaidi na Mwenyekiti wa Tawi hilo Mijo Laizer
NA MWANDISHI WETU, MOSHI
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amedai kuzinasa nyaraka za zinazosambazwa na CHADEMA nchi nzima kuchochea maandamano na kuzuia wananchi kuchangia shughuli za maendeleo nchi nzima.
Akizungunza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye Stendi Kuu ya mabasi mjini Moshi, Nape alisema, nyaraka alizonasa ni pamoja na baruza yenye kumbukumbu namba CDM/DSM/HU/Vol 040/2011 ya Julai 20, 2011, ambayo CHADEMA imewasambazia wenyeviti wa chama hicho kila mkoa kuchoandaa maandamano nchi nzima baada ya kikao cha Bunge la bajeti.
Kwa mujibu wa Nape barua hiyo ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CAHDEMA, Erasto Tumbo barua hiyo inashinikiza wenyeviti hao kutekeleza maamuzi ya Kamati Kuu ya chama hicho kuandaa maandamano hayo ili kuiwaibisha serikali kwa madai kwamba imeshindwa kutekeleza majukumu ya kuwaletea maendeleo wananchi.
“Ni jukumu lako Mwenyekiti na makatibu wa majimbo katika mikoa kuanza kuhamasisha wananchi na kupanga wafuasi kikamilifu kwani harakati za awamu hii ni ndefu sana baada ya vikao vya bunge”, Nape alinukuu sehemu ya barua hiyo ambayo aliionyesha katika mkutano huu.
Alisema barua nyingine ni yenye kumbukumbu namba CDM/DSM/ Vol. 138/2011 ya Juni 30,2011 ambayo pia imesainiwa na Tumbo iliyosambazwa kwa Makatibu wa Majimbo kutakiwa kutekeleza agizo la Kaatibu Mkuu wa CHADEMA Wilborod Slaa kuhamasisha wananchi wagome shughuli za maendeleo.
Barua hiyo ambayo Nape aliionyesha mkutanoni ina kichwa ‘ Utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu kuhamasisha wananchi wagome kuchangia shughuli za maendeleo”.
“”Unatakiwa kutekeleza agizo la Katibu Mkuu (Wilbrod Slaa) kuhamasisha wananchi wagome kuchangia shughuli za maendeleo …Tayari mhe. Katibu Mkuu keshafanya hivyo majimbo kadhaa hasa kule Songea ambapo muzimu huo unaitafuna serikali ya CCM na wabunge” Nape alikariri sehemu ya barua hiyo yenye ukurasa mmoja.
Nape aliwataka wananchi kote nchini kukaataa kuingia kwenye mtego wa CHADEMA ambao alisema wanauandaa kwa sababu hawana uchungu na nchi, wanataka wananchi wache kuchangia maendeleo na badala yake watumbukie katika maandamano ambayo hayatawapa faida yoyote badala ya kuwaongezea dhiki.
Alisema, wakati Chadema watataka kuhamaisha wananchi kutochangia shughuli za maendeleo , wananchi wenyewe ni mashahidi kwamba yapo mafanikio mengi ambayo yamepatikana katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na uchangiaji.
Nape alitaja moja ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na uchangiaji kuwa ni ujenzi wa shule za sekondari za Kata, ambazo kutokana na kujengwa kwake sasa waatoto wengi wamepata fursa ya kwenda shule.
Kabla ya kuhutubia mkutano huo, Nape alifungua shina la wana-CCM wapya lililoundwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Tumaini cha Kumbukumbu ya Mtakatifu Stephano (SIMCO) kilichopo Mwika, Moshi Vijijini ambapo jumla ya wanachama wapya 108 wa CCM walikabidhiwa kadi.
Akizungumza naa wasomi hao katika kutano uliofanyika katika ukumbi wa King Size, Himo, Nape aliwataka wanafunzi kutambua kwamba siasaa siyo ajira bali ni tunu ambayo humtokea mtu baadaye baada ya kufanya maandalizi katika mambo mengine.
Aliwataka kutoingia katika siasa kwa lengo la kuifanya ndiyo ajira yao kwa kuwa kufanya hivyo wakati bado wapo masomoni haatafanikiwa vyote kwa kuwa ni rahisi kuanguka kimasomo mtu atakapogeuza siasa kuwa mradi.
Nape aliwataka wanafunzi waliofungua tawi kuwa chachu ya mabadiliko ndani ya chama na sikwa lengo la kutafuta vyeo kama ambavyo wengi wanadhani.