Sababu Kuu Tatu zinazopelekea Ndoa Kuvunjika!

NDOAYATHEA-778292

NDOA ya mastaa wa filamu Bongo, Mike Sangu ‘Mike’ na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ (Picha kwa hisani ya Mwanajamii wa Kweli)

 

Mtaalam wa masuala ya mapenzi na ndoa, Timothy Scheiman, anasema Talaka [divorce] huwa zinatokea na tofauti huwa ni nyingi zisizo na muafaka [irreconcilable differences], lakini talaka nyingi hutokea chini ya sababu kuu tatu, ambazo zinatokana na; kujamiiana; fedha; ndugu, jamaa, na marafiki. Scheiman anaendelea kuzichambua sababu hizo kuu tatu kama ifuatavyo:

Kujaamiiana (Sex)

Mtaalam anasema, kujaamiiana kumekuwa ni chanzo kikuu cha kwanza kwa ndoa nyingi kuvunjika. Iwe ukosefu wa kujamiiana, kujamiiana kidogo, ukosefu wa elimu kuhusu tendo zima la kujaamiiana, au kujaamiiana na mtu ambaye hakukusudiwa (wrong person). Scheiman anaendelea kusema kwamba inamshangaza sana kuona watu wanaingia kwenye ndoa wakati ufahamu wao wa tendo la ndoa uko chini sana. Pamoja na hilo, anaonya kwamba hii sio sababu ya watu kufanya majaribio kwanza kabla ya kuoana (experiment before marriage), bali ni kwa wana ndoa kusoma vitabu, kuulizana na kuzungumza kuhusu vile vinavyowapendeza na kuwavutia katika tendo hilo muhimu, ili kuridhishana. Kwa maneno mengine, mke atafute kipi kinachomridhisha (please) mume, na alkadhalika mume atafute kipi kinachomridhisha mke.

Zaidi anasema, hofu na kutokujua huweza kusababisha matatizo makubwa katika ndoa. Pia, kulazimisha mshirika mmoja (partner) kushiriki kwenye mitindo na matendo (positions and acts), ambayo haipendi au kukubaliana nayo, pia inasababisha matatizo makubwa. Anashauri wana ndoa wawe makini na wawazi zaidi katika mawasiliano yao, ili kuepuka hii sintofahamu. Kwa msaada zaidi, anapendekeza wanandoa wasome kitabu kiitwacho “The Act of Marriage” kilichoandikwa na Tim Lahaye. Anasema kitabu hiki kina mandhali ya kikristo, lakini hakifichi kitu inapokuja suala la kujaamiiana. Ana amini kwamba kama wanandoa watajieleimisha, basi matatizo yatapungua katika nyanja hii.

Fedha (Finance)

Hapa mtaalam ana anza na ovyo kali kwamba moja kati ya vitu ambavyo vinaweza vikateketeza ndoa ni malumbano kuhusu fedha. Wakati wanandoa wana madeni au wanalumbana fedha kiasi gani imetumika au kuhifadhiwa, kunaweza kukatokea matatizo makubwa. Katika suala hili, mtaalam anashauri wanandoa wafanye yafuatayo:

  1. Wasijiingize kwenye madeni makubwa , na kama mpo kwenye madeni sasahivi, basi huu ni wakati muafaka wa kujipanga na kujinasua kwenye madeni hayo.
  2. Ana amini Bajeti mara nyingi hazitekelezeki kwenye ndoa, lakini anashauri angalau kuwepo makubaliano baina ya wanandoa kwamba matumizi yeyote yanayozidi $100 (ni kama 160,000 za Kitanzania) yapate baraka za wanandoa kabla ya kuhidhinishwa.
  3. Kila mshirika katika ndoa awe na fedha “ kichaa” kidogo (mad money) za kutumbua kutoka katika kila malipo ya wiki (kwa wale wa Bongo malipo ya kila mwezi) angalau hata shilling chache au tudola kadhaa. Lengo hapa ni kuwa na uhuru wa kuzitumia pesa hizo utakavyo, nje ya makubaliano yaliyotajwa hapo juu.
  4. Mwisho, wanandoa lazima wahakikishe kwamba wanahifadhi pesa zao (saving) hata kama kiasi kidogo kwa week, kwani kikidundulizwa kiasi hicho kinakuwa kikubwa mbele ya safari.

 

Ndugu, jamaa, na marafiki

Mtaalam anatahadharisha kwamba hao watu waliotajwa hapo juu wanaweza wakawa sumu katika ndoa kama mwanandoa hayupo makini. Watu wao waliotajwa wanahusisha pia mama, baba, madada, makaka, na kadhalika. Hawa si washirika katika ndoa, ndoa ni ya watu wawili tu,yaani mke na mume. kwahiyo hao watu lazima wawe na mipaka katika ndoa yako. Kama utawaruhusu watu wao wazungumze wanachotaka kuhusu mwenza wako au ndoa yako, basi ujue unaelekea kuizika ndoa yako, ana malizia kusema mtaalam.

 

Wewe una maoni gani kuhusu hizi sababu za uvunjifu wa ndoa? Je unafikiri hizi sababu zina mashiko yeyote katika jamii yetu ya Kitanzania?

 

 

Imeandaliwa na: www. thehabari.com

 

 

Chanzo: Yahoo Voices