Kiongozi UVCCM Awasaidia Vifaa Mabondia Kinondoni

Rehema Mbegu (kulia) akikabidhi vifaa kwa mabondia wa kambi ya Bigright ya Mwananyamala.

Rehema Mbegu (kulia) akikabidhi vifaa kwa mabondia wa kambi ya Bigright ya Mwananyamala.


Hata mimi naweza inaonekana akisema Rehema Mbegu ngumi ni mchezo wa wote, hapa akizipiga na bondia Martin Shekivuli.

Hata mimi naweza inaonekana akisema Rehema Mbegu ngumi ni mchezo wa wote, hapa akizipiga na bondia Martin Shekivuli.

Na Mwandishi Wetu
 
MGOMBEA wa nafasi ya ukatibu UVCCM, Jimbo la Kinondoni, Rehema Mbegu leo amewazawadia mabondia wa kambi ya Bigright ya Mwananyamala vifaa vya michezo zikiwemo bukta za ulingoni jozi nane za gloves, vilinda chini (groin guard) na vilinda kinywa kwa mabondia.

Rehema Mbegu ambaye kwa sasa ni Katibu wa UVCCM Kata ya Mwananyamala na Kiongozi wa Timu ya Garden Queen ya Kinondoni alitoa vifaa hivyo baada ya kuombwa kwa muda mrefu na vijana hao kwamba awasaidie vifaa hivyo kama mlezi wao.

Akizungumza na wanahabari, Rehema Mbegu alisema kuwa kutoa ni moyo na wala si utajiri, na niwajibu wa viongozi kusaidiana katika sekta mbalimbali, hivyo kwa kuwa yeye hana uwezo mkubwa wa kuwatosheleza kwa kila kifaa cha mazoezi. “Natoa hivi vichache viwasaidie na kila nipatapo uwezo sitawaacha nitakuwa nanyi pamoja kama ilivyo sasa, naamini na wengine wenye uwezo nimewafungulia njia wajitokeze kuwasaidia mabondia wetu,” alisema.

“Nawaomba wadau wengine wa michezo, wasiwatenge wanamichezo hasa mabondia, kwani ngumi ni mchezo mgumu na vifaa vyake ni ghali hivyo mabondia wenyewe hawawezi kumudu kutokana na kipato chao kidogo…tuwasaidie vijana wetu ili tuwaokoe na majaribu ya madawa ya kulevya na mambo mengine ya kihuni kama wizi, ukabaji na mengineyo hatari,”

Naye kiongozi wa Bigright Boxing ya Mwananyamala amemshukuru Mbegu kwa msaada wa vifaa hivyo na kuahidi wata hakikisha wanavitunza na kuvitumia vizuri, ili viwasaidie vijana wengi. “…Tumepata vifaa hivi katika muda muafaka hasa kipindi hiki cha mashindano  mfululizo yaliyo mbele yetu, kwa mfano bondia wetu Issa Omari Nampepeche anatarajiwa kucheza na bondia toka Tanga Zuberi Kitandula Machi 29 katika pambano la raundi sita kuwasindikiza mabondia Japhet Kaseba atakaye minyana na Thomas Mashali kugombania ubingwa wa UBO katika ukumbi wa PTA sabasaba, hivyo vifaa hivi vichache vitatusaidia sana katika mashindano haya yanayotukabili tufanye vizuri,” alisema.