Msanii Yusuph Mlela Awasaidia Vifaa Mabondia Kinondoni

Msanii wa filamu nchini, Yusuph Mlela kushoto akikabidhi baadhi ya vifaa vya mchezo wa ngumi kwa kocha wa klabu ya Msisiri, Daudi Muhunzi ikiwa ni uboreshaji wa klabu hiyo iliyopo CCM Msisiri Kinondoni Dar es salaam, wa pili kulia ni Ally Moja na Rashid Kipaga.

Msanii wa filamu nchini, Yusuph Mlela kushoto akikabidhi baadhi ya vifaa vya mchezo wa ngumi kwa kocha wa klabu ya Msisiri, Daudi Muhunzi ikiwa ni uboreshaji wa klabu hiyo iliyopo CCM Msisiri Kinondoni Dar es salaam, wa pili kulia ni Ally Moja na Rashid Kipaga.


Na Mwandishi Wetu

MSANII wa filamu za bongo, Yusuph Mlela ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya mchezo wa masumbwi nchini na kuvikabidhi kwa klabu ya mchezo huo inayojulikana kwa jina la Msisiri iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya vifaa vilivyotolewa na msanii huyo ni pamoja na Gloves, clip bandage, Protector, Gumshit. Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa hivyo Mlela alisema amevutiwa na kitendo cha vijana wa kambi hiyo wanavyojituma kufanya mazoezi hivyo akaamua kujitolea kidogo alichonacho kwa ajili ya kuendereza mchezo huo wa masumbwi nchini.

“…Katika kata ambayo mimi naishi karibu na maeneo haya walijitokeza pia kuniomba nichangie nikawa sina jinsi kwa kuwa na mimi siku moja moja nitakuwa nakuja kufanya mazoezi hapa hapa nawaomba wadau wengine wenye uwezo zaidi yangu wasaidie vijana kwa ajili ya kujiendeleza na mchezo huu waupendao,” alisema.

Kwa upande wake kocha wa mchezo wa ngumi katika klabu ya Msisiri, Daudi Muhunzi alitoa shukrani kwa Mlela kwa kitendo cha kuwakumbuka vijana wenzie ambao wana uhaba wa vifaa vya mchezo wa ngumi kwani yeye amekuwa kama mkombozi katika kata hiyo.

“…Tunaomba wadau wengine waje watusaidie vifaa mbalimbali kama punch bag, pad na masuala ya udhamini wa muda mrefu kwa ajili ya kuendeleza kambi hii ya mazoezi ‘gym’ ambayo tunaitumia kwa kuchangia kidogo,” alisema.