Usichokijua Kuhusu Afya Yako na Dk Ally Mzige, Mazoezi Huongeza Nguvu za Kiume/Kike..!

Dk. Ally Mzige kutoka kliniki ya mazoezi tiba Mikocheni "A' akizungumza na waandishi wa habari leo.

Dk. Ally Mzige kutoka kliniki ya mazoezi tiba Mikocheni “A’ akizungumza na waandishi wa habari leo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Dk. Mzige leo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Dk. Mzige leo.

Dk. Ally Mzige kutoka kliniki ya mazoezi tiba Mikocheni "A' akizungumza na waandishi wa habari leo. Kulia ni mmoja wa maofisa wa idara ya habari maelezo Dar es Salaam.

Dk. Ally Mzige kutoka kliniki ya mazoezi tiba Mikocheni “A’ akizungumza na waandishi wa habari leo. Kulia ni mmoja wa maofisa wa idara ya habari maelezo Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

WATU wengi hawapendi kufanya mazoezi japokuwa yanaumuhimu mkubwa kwa mwili wa binadamu. Dk. Ally Mzige anasema mazoezi ya viungo kwa mwili wa binadamu hasa yanayofanywa asubuhi yana faida 30. Akifafanua zaidi anazitaja faida za mazoezi ya viungo kuwa ni pamoja na husaidia kuongeza nguvu za kiume kwa mwanaume na nguvu za kike kwa mwanamke, humsaidia mtu kupunguza uzito na kuimarisha mifupa, humpunguzia binadamu uwezekano wa kupata BP, pia hupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa pumu na hupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari.

Anazitaja faida zingine za kufanya mazoezi humpunguzia mtu kuzeeka mapema, mazoezi hukuongezea uwezo wa kufanya tendo la ndoa, husaidia kuufanya mzunguko wa damu kutiririka vizuri mwilini, mazoezi humpunguzia mtu kupata mshtuko au kupooza.

Anasema kwa wavutaji sigara wanahatari zaidi kwani kilevi hicho kina kemikali 4000 ambazo ni hatari kwa mwili wa mtumiaji na kibaya zaidi kati ya kemikali hizo 60 ndizo zinaleta magonjwa ya kansa mbalimbali kwa mtumiaji. Anasema kwa watumiaji wa mirungi wana hatari zaidi kwani mbali na kuwa na madhara mengine kiafya mirungi humpotezea mtumiaji hisia za kufanya tendo la ndoa.

Dk. Mzige anasema mirungi ina kemikali 1500 tofauti na bangi ambayo ina kemikali 400. Hata hivyo anasema bangi inamadhara mengine zaidi ya uwepo wa kemikali hizo kwani endapo mtu anavuta bangi na bado haja balee basi anatengeneza homoni za kike mwilini kwake hivyo anaweza kujikuta anatabia za kike.