Ridhiwani Kikwete Ahaidi Neema Chalinze, Kila Kijiji Kupewa Matrekta

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Msigi, Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze Machi 18,2014. Picha na Othman Michuzi.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene, Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014. Katika Mikutano yake kwenye Vijiji vya Mindukene, Msigi na Kisanga ndani ya Jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo. Picha na Othman Michuzi

Na Mwandishi Wetu, Chalinze

MGOMBEA wa Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo kiwe natija.
Mgombea huyo ametoa ahadi hiyo wakati wa mikutano ya kampeni kwenye vijiji vya Mindukene, Msigi na Kisanga vyote vikiwa kwenye Kata ya Talawanda.

Kikwete alisema kuwa wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono ambalo haliwezi kuwaletea manufaa wala kuboresha kilimo ambacho ni tegemeo lao.

“Nikifanikiwa kupata ubunge nitahakikisha kila kijiji kinakuwa na matrekta kwa ajili ya wakulima ambao wataweza kulima kwa faida kwa ajili ya chakula na ziada kuuza ili kujiongezea kipato,” alisema Kikwete.

Akizungumzia changamoto ya migogoro ya wakulima na wafugaji alisema kuwa atahakikisha anazikutanisha pande zote ili kujua chanzo cha migogoro hiyo na namna ya kuitatua.

“Tatizo kubwa ni viongozi kushindwa kuzikutanisha pande zinazohusika badalayake wanaongea na upande mmoja jambo ambalo haliwezi kumaliza migogoro hiyo, …njia pekee ni kuwa na matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo kwa wakulima na wafugaji,” alisema Kikwete.

Aidha aliongeza kuwa migogoro hiyo inatokana na wafugaji kuingia kinyemela pasipo kufuata taratibu bila ya kupitia kwenye mikutano mikuu ya serikali za vijiji. Katika hatua nyingine aliwataka wazazi kuepukana na tabia ya kuuza kiholela maeneo yao hali ambayo itasababisha vijana kukosa ardhi kwa ajili ya kilimo na makazi.

Aliongeza kuwa atahakikisha anaboresha masuala mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, afya, miundombinu, kilimo, mikopo kwa vijana na akinamama, uzinduzi rasmi wa kampeni unatarajiwa kufanyika kesho Aprili huko Chalinze na uchaguzi utafanyika Aprili 6 mwaka huu.