Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea Jogoo kutoka kwa kina Mama wa Kijiji cha Kwamsanja, Kata ya Kibindu Machi 16,2914. Picha na Othman Michuzi
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete wapungua mkono wananchi wa Kijiji cha Kwarihombo, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Kijiji hicho, Machi 16,2014. Picha na Othman Michuzi.
Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM), Steven Kazidi akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Kijiji cha Kwarihombo, Kata ya Mbwewe, Bagamoyo Machi 16,2014. Picha na Othman Michuzi.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM), Steven Kazidi wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja dogo katika Kijiji cha Chang’ombe, linalounganisha Barabara inayotoka Kwarihombo kupitia Kwamsanja mpaka Kibindu, Kata ya Kibindu, ndani ya Jimbo la Chalinze Machi 16,2015. Picha na Othman Michuzi.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza kwa makini Mlemavu wa miguu, Hamis Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Kwarihombo, ambaye alikuwa akimuomba Mgombea huyo msaada wa kupatiwa Baiskeli ya kutembelea kutokana na kwamba aliyonayo imechoka sana. Ridhiwani ameahidi kumpelekea Baiskeli mpya ya kutembelea mlemavu huyo. Picha na Othman Michuzi.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa ameungana na wananchi wa Kijiji cha Kwamduma,Kata ya Kibindu kwenye Msiba wa Mtoto wa Mzee Juma Mkonje (hayupo pichani) uliotokea Machi 16,2014.