KATIBU Mkuu Kiongozi, Phillemon L. Luhanjo amemteua Eliakim Chacha Maswi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.
Luhanjo amefanya mabadiliko hayo jana baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, David Jairo, kupewa likizo kwa muda, ili kupisha uchunguzi katika ofisi yake, ambapo inadaiwa wizara hiyo ilizichangisha fedha taasisi zake kwa lengo la kutumika kushawishi bajeti ya wizara ipitishwe na wabunge.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozie Julai 22, mwaka huu; inaeleza Luhanjo, amemteua ELIAKIM CHACHA MASWI, kuwa KAIMU KATIBU MKUU, Wizara ya Nishati na Madini kushika nafasi ya Jairo. Maswi kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.