Cosmas Njingo-afisa habari na mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro akichangia mada.
Zadock Kitomary-Mkulima bora mara mbili mfululizo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha akitoa mada.
Ayubu Nnko-Msimamizi wa Jarida kwa upande wa Tanzania akitoa mada katika Semina hiyo.
Coroline Nyakundi- Meneja Mradi The Organic Farmer& jarida la Mkulima mbunifu akitoa mada.
John Cheburet-Mtayarishaji wa vipindi vya Redio kutoka jarida la Mkulima mbunifu .
******
IMEELEZWA kuwa Watanzania ni wavivu wa kusoma majarida mbalimbali yanayoweza kuwaongezea upeo ukilinganisha na nchi zingine. Hayo yamebainishwa na Mmoja wa maofisa wa Jarida la Mkulima Mbunifu, Caroline Nyakundi kutoka nchini Kenya, wakati akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari za kilimo na wataalamu wa kilimo yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Arusha Crown ya Mjini hapa.
Ameongeza kuwa kunatofauti kubwa ya Mwitikio wa kusoma machapisho kati ya Raia wa Tanzania ukilinganisha na Kenya ambako imeelezwa kuwa wanauhitaji mkubwa wa kujifunza mbinu mpya za
kilimo tofauti na Watanzania ambao hawana uhitaji wa kusoma na kutaka kujua zaidi.
kilimo tofauti na Watanzania ambao hawana uhitaji wa kusoma na kutaka kujua zaidi.
Akieleza Mikakati ya Jarida la Mkulima Mbunifu mmoja katika ya Maafisa wa Jarida hilo, Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya, amesema tangu kuzinduliwa kwa jarida hilo Juni, 2011 limeonesha
mwitikio mkubwa kutokana na kupata taarifa nyingi kutoka kwa wakulima wakilihitaji ili kujua zaidi habari za Kilimo.
mwitikio mkubwa kutokana na kupata taarifa nyingi kutoka kwa wakulima wakilihitaji ili kujua zaidi habari za Kilimo.
Amesema Jarida hilo limelenga zaidi maoni na mahitaji ya Mkulima kutokana na mawazo yao ambayo wamekuwa wakiyatoa katika jarida hilo mara kwa mara jambo linaloonesha Mkulima kufikiwa na Jarida hilo na kwa wakati. CHANZO; Arusha Yetu Blog