DTBi-COSTECH na SVCED Waingia Mkataba

Bw. Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi kupeana mikono baada ya kusaini MOU.

Bw. Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi kupeana mikono baada ya kusaini MOU.

Mr Carl Davis Jr, President of the Silicon Valley Black Chamber of Commerce and Eng. George Mulamula, CEO of DTBi sign MOU copy

Bw.Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi (kulia) wakisaini MOU.

KAMPUNI tanzu ya Tume ya sayansi na teknolojia ya DTBi-COSTECH na Silicon Valley Black Chamber of Commerce’s Center for Entrepreneurial Development (SVCED) wametiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano (MoU) ambapo pande zote mbili zitashirikiana kwa njia mbalimbali kwa ajili ya ukuaji wa wajasiriamali.

Mkataba huo, kati ya DTBi na SVCED utawezesha pande hizo mbili kukuza ujasiriamali na kujenga uwezo katika Habari, Teknolojia na Mawasiliano kwenye sekta zote za kiuchumi.

Mkataba huo wa MoU utawafanya wadau kufanya shughuli za biashara kwa kuanza na mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kupitia njia ya mtandao na kusaidia wale walio na ubunifu katika nyanja mbalimbali za biashara.

Mkataba huo pia utasaidia wajasiriamali kuweza kukua na kufanya biashara kwa kutumia mifumo habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza ujasiriamali na kuanzisha mfumo wa kubadilishana uzoefu katika kuendeleza biashara na ukuaji wa ujasiriamali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi,  Injinia. George Mulamula amesema mkataba MOU utatoa ushirikishiano ambao utaruhusu wajasiriamali wa Tanzania kufaidika na ujuzi, maarifa  ya Silicon Valley ya ujasiriamali.

Amesema hii itasaidia nchi ya Tanzania kuruhusu uanzishwaji wa biashara kupitia njia ya mtandao na mifumo ya Habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza ajira na kuchangia pato la taifa.

Mr Mulamula explains the partnership to the press copy

Eng.George Mulamula akielezea ushirikiano kwa vyombo vya habari.

Baada ya kutiliana saini ya MOU, Bw Carl Davis Jr, alikuwa na semina kwa wajasiriamali yenye jina la “The Mindset of the Silicon Valley Entrepreneur: Lessons for the Tanzania Entrepreneur/Innovator”.

Mr Davis Jr amesema anaweza kuwasaidia “wajasiriamali kuelewa jukumu la uzinduzi na ujasiriamali na jinsi Wajasiriamali hapa nchini jinsi wanavyoweza kujiinua katika kufikiri chanya kwenye maeneo ya biashara.

Mr Carl Davis Jr,  gives a talk to Tanzanian entreprenuers at DTBi copy

Bw. Carl Davis Jr, akitoa majadiliano DTBi kwa wajasiriamali wa Tanzania juu ya jinsi ya kuwa mwekezaji mwenye mafanikio.

Attendee contributing to the discussion copy

Mshiriki akichangia mjadala. CHANZO; MOblog Tanzania