Sanya Juu ni mji mdogo ndani ya wilaya Siha Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni Km 25 toka Bomang’ombe na KM 50 toka Moshi Mjini, weekend hii nilifanikiwa kuutembelea Mji wa Sanya Juu ambapo siku ya Jumamosi mji huu huwa umechangamka kwa shamrashamra za kibiashara. katika pita pita zangu nilifanikiwa kulitembelea soko ila nilishangazwa na hali niliyo ikuta ya miundombinu isiyo kidhi na kulifanya soko kuonekana hatarishi kwa wafanyabiashara na wateja wao kiafya. Huu ni msimu wa mvua kwa sehemu kubwa ya mkoa wa Kilimanjaro, hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa kuimarisha miundombinu ya soko la Sanya Juu kuimarisha afya za wafanyabiashara na wateja wao.
|
Hii ni njia ya kuelekea soko hili ikiwa imejaa matope kutokana na kuwa katika kiwango cha changarawe. |
Baadhi ya wachuuzi wakiwa sokoni hapo kununua mahitaji yao lakini mazingira ya soko hayaridhishi kutokana na uchafu uliokithiri hapo na kuhatatrisha afya za walaji wa bidhaa |
hali halisi inavyonekana sokoni hapo baada ya mvua kunyesha |
Msimu huu wa mvua unasababisha kero hii kwa baadhi ya wateja hata wafanyabiashara sokoni |
Hali hii pia ni kero kwa watembea kwa miguuu sokoni hapo. |
Picha zote na mdau Wito Msafiri wa Mwanaharakati Mzalendo Blog |