Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa baada ya kuwasili katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru mwakilishi wa UNICEF nchini kwa mchango wa dola za kimarekani 100,000 huku Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa wakishuhudia katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Bi. Lucy Kimei kwa kuwasilisha shilingi milioni tatu kama mchango wa familia ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk. Charles Kimei katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Rais mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa akimshukuru mwakilishi wa taasisi ya WAMA Bi. Caroline Mthapula kwa mchango wa taasisi hiyo katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Februari 22, 2014, aliongoza harambee ya kupatikana kwa zaidi ya sh milioni 600 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya matibabu kwa ajili ya Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Dar Es Salaam.
Katika halfa hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Dar Es Salaam, Rais Kikwete pia ameahidi kuendeleza kuongoza jitihada za kupatikana kwa kiasi cha sh milioni 328 ambazo zinahitaji kukamilisha hesabu ya sh. 929, 915,000 ambazo ndizo zilikuwa lengo la halfa ya jana.
Halfa hiyo pia iliwakutanisha viongozi wakuu wa awamu tatu za uongozi wa juu wa Tanzania ambako Rais wa Pili wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Tatu za Tanzania, Mzee Benjamin William Mkapa walikuwa wenyeji wa halfa hiyo kwa nyadhifa zao kama walezi wa Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania (PAT).
Uchangiaji katika halfa hiyo ulikuwa wa aina tatu – kuna fedha taslimu milioni 55.4 zilizochangwa moja kwa moja, kuna ahadi za uchangiaji na kuna wachangiaji walioamua kuwa watatoa fedha za kununua vifaa mbali mbali vinavyohitajika katika Wodi hiyo ambayo gharama yake inakadiriwa kufikia dola za Marekani 570,500.
Katika halfa hiyo, Ikulu ya Rais Kikwete imetoa mchango wa kununua mashine iitwayo Infant Radiant Warmer yenye thamani ya dola za Marekani 15,300 wakati Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mama Salma Kikwete imechangia ununuzi wa mashine iitwayo Compressor Nebulizer ambayo gharama yake ni dola za Marekani 12,000.