Na Mwandishi Wetu
MATOKEO ya Kidato cha nne kwa 2013 yametangazwa huku watahiniwa 235,227 wakifaulu mtihani huo ikiwa ni sawa na asilimia 58.25 ya waliofanya mtihani huo. Jumla ya wanafunzi 404,083 walifanya mtihani huo huku waliofaulu kwa daraja la I-III wakiwa wanafunzi 74,324 sawa na asilimia 21.09 ya waliotahiniwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Balaza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo jijini Dar es Salaam, shule 10 za sekondari zilizofanya vizuri (zilizoongoza) ni pamoja na St. Francis Girls, Marian Boys, Feza Girls, Precious Blood, Canossa, Marian Girls, Abbey, Anwarite Girls, Rosmini na Don Bosco Seminary.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa shule kumi za sekondari zilizofanya vibaya zaidi ni pamoja na Singisa Sekondari, Sekondari ya Hurui, Sekondari ya Barabarani, Sekondari ya Nandanga, Sekondari ya Vihokoli, Sekondari ya Chongoleani, Sekondari ya Likawage, Sekondari ya Gwandi, Sekondari ya Rungwa na Sekondari ya Uchindile.
Ilifafanua zaidi kuwa kati ya watahiniwa 404,083 waliofanya mtihani wasichana waliofaulu ni 106,792 huku idadi ya wavulana waliofaulu ikifikia 128,435. Wavulana waliopata daraja la kwanza (division one) ni 5,030 huku idadi ya wasichana ikiwa ni 2,549.
Aidha wavulana waliopata daraja la tatu (division three) ni 27,904 na wasichana ni 17,113. Wanafunzi waliopata daraja la nne (division four) ni 126,828, huku idadi ya wasichana wakiwa 62,841 na wavulana 63,987.
Taarifa imefafanuwa kuwa jumla ya wanafunzi 151,187 wamepata sifuri (division ziro), ambapo idadi ya wasichana ni 72,237 na wavulana ni 78,950. Taarifa zaidi za matokeo haya endelea kufuatilia mtandao wa dev.kisakuzi.com.