DC Asema Mbinu za Kisasa Zinahitajika Kuelimisha Jamii

Mkufunzi wa Teknolojia ya simu kwa habari kutoka Chuo Kikuu, Bi. Faith Shayo akifafanua  jinsi simu za “SMART” zinavyoweza kutumika kwa habari mbalimbali, picha na maoni kutoka na kwenda katika jamii kupitia maelekezo husika yaliyomo katika simu.

Mkufunzi wa Teknolojia ya simu kwa habari kutoka Chuo Kikuu, Bi. Faith Shayo akifafanua jinsi simu za “SMART” zinavyoweza kutumika kwa habari mbalimbali, picha na maoni kutoka na kwenda katika jamii kupitia maelekezo husika yaliyomo katika simu.

 

Na Mwandishi Wetu

DEMOKRASIA vijijini itapatikana iwapo vyombo vya habari jamii vitatumika kikamilifu na kutekeleza wajibu wake wa kupasha habari kwa kutumia teknolojia mpya.

Akifungua mafunzo ya wiki moja katika Ukumbi wa Mazingira, Kibaoni Ifakara yanayowashirikisha wanahabari jamii kutoka Pemba, Unguja, Pangani, Ifakara na Kyela, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Hassan Masala amesema mbinu za kisasa zinahitajika kuelimisha jamii na mambo gani yafanyike ili kupata uongozi bora vijijini na taifa kwa ujumla.

Bwana Masala amesema pamoja na changamoto zilizoko vijijini, Redio Jamii Pambazuko iliyoko Ifakara, ina mchango mkubwa katika kuelimisha na kukuza demokrasia katika wilaya ya Kilombero kwa kuwa inafika sehemu kubwa ambako serikali haifiki kwa urahisi.

Amesema kutokana na miundo mbinu mibovu ya usafiri, mafunzo ya matumizi ya simu kwa kiasi kikubwa yataongeza ujuzi katika taaluma ya upashaji habari.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 7 mwezi Februari 2014 yanalenga kutambua uwezo wa simu katika kutafuta na kutoa habari, kujifunza jinsi Tehama inavyorahisisha mawasiliao kwa njia ya simu aina ya “SMART” na kuboresha mbinu za upatikanaji na utoaji wa habari.

Mafunzo ya Tehama kwa redio jamii ni mwendelezo wa mradi wa kuzipatia uwezo redio hizo kwa kutumia teknolojia mpya unaofadhiliwa na UNESCO kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA).

DSC_0397

Mkufunzi na Mtaalamu wa Masuala ya Redio Jamii Mama Rose Haji Mwalimu kutoka UNESCO, akieleza madhumuni ya mafunzo kwa washiriki, katika Ukumbi wa Mazingira Kibaoni, Ifakara.

20140204_155711

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya TEHAMA kutumia simu kwa mawasiliano wakifanya kazi za vikundi.

20140204_155841

Washiriki katika vikundi kazi wakitumia simu zao kufanya mazoezi kutokana na mafunzo waliyopata kwa mawasiliano rahisi vijijini.

IMAG0275

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi pamoja na washiriki wa Redio Jamii kutoka Pangani, Pambazuko, Kyela, Pemba na Unguja.