JK Awataka WanaCCM Kukabiliana na Fujo za Chadema

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. Jakaya Kikwete, akifungua rasmi Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichoanza jioni hii kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Picha na OMR

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. Jakaya Kikwete, akifungua rasmi Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichoanza jioni hii kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Picha na OMR

2(4)
JK Awataka WanaCCM Kukabiliana na Fujo za Chadema
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Balozi Ali Mchumo (kushoto) Bernad Membe  (kulia) na Adam Malima, wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa kikao hicho.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Balozi Ali Mchumo (kushoto) Bernad Membe 
(kulia) na Adam Malima, wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa kikao hicho.

Ni Wajumbe wa CCM waliohudhuria kikao hicho.

Ni Wajumbe wa CCM waliohudhuria kikao hicho.

Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mjumbe mwenzake Edward Lowassa, wakati alipokuwa akiingia kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, Feb 15, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Picha na OMR

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika jengo la White House mjini Dodoma, akiwa meza kuu na Makamu wa Rais wa CCM visiwani na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. PICHA NA IKULU.

Na Bashir Nkoromo

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amewapa rungu wana-CCM akiwataka kuacha kujifanya wanyonge dhidi ya vitendo vya fujo ambavyo hufanyiwa na Chadema hasa nyakati za uchaguzi. Rais Kikwete amesema hayo wakati akiongoza kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini Dodoma.

“Uchaguzi wa Kalenga ndiyo huo upo mbele yetu, hadi sasa hakuna tatizo lililojitokeza kama Arumeru mambo yapo shwari kabisa, lakini tujue tu kwamba pale tunaenda kushindana na watu (Chadema) ambao wao silaha yao ya kwanza ni fujo…ninaagiza sasa lazima wana CCM kukabiliana na fujo zao. Unyonge basi.”, alisema Rais Kikwete na kuongfeza;

“CCM kuendelea kujifanya wanyonge kila mara sasa basi. Haiwezekazi watu wanafanya vujo hadi kuwatoboa watu macho ninyi nmanyongea tu, hili haliwezekani. Tazama pale Ingunga  mtu wenu alimwagiwa tindikali hadi leo ana  ulemavu wa kudumu kisa uchaguzi tu, aah haiwezekani kabisa,” alisema Rais Kikwete.

Mapema Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete alipongeza wana CCM na viongozi wao katika Kata zote zilizofanya uchaguzi mdogo wa Udiwani na hatimaye CCM kuibuka na ushindi wa Kata 23, Chadema ikiambulia tatu na NCCR Mageuzi kimoja.

Hata hivyo Rais Kikwete alisema, licha ya CCM kuzoa kata nyingi kwenye uchaguzi huo, viti vinne kwenda kwa upinzani bado ni doa hivyo lazima CCM ihakikishe inazikomboa kata hizo nyakati za chaguzi zijazo.

“Ni kweli tumezoa kata nyingi, lakini kwa kuwa lengo letu CCM kila wakati ni kushinda tu, hatua hiyo ya kuzikosa kata nne bado ni doa lazima kuzikomboa kata hizo chaguzi zijazo,” alisema, Rais Kikwete.

Pia alipongeza CCM kwa ushindi iliopata kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Kimbesamaki na kwamba CCM inaona fahari kulirejesha jimbo hilo mikononi mwake, kwa kuwa ilikuwa imelazimika kumfukuza mwakilishi wake wa awali kwenye jimbo hilo kwa usaliti aliyefaa kuendelea kuwemo ndani ya chama.