Bia ya Serengeti Yaendesha Droo ya Kwanza ya Winda Safari ya Brazil

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Serengeti Allan Chonjo akiongea kwa njia ya sinu na moja wa washindi wa droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti iliyochezeshwa mapema leo jijini Dar es Salaam kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo. Ambapo washindi wawili wamejishindia 'Samsung tablets' ambao ni Mwl. John Yesaya (49) kutoka mkoani Kilimanjaro na Salehe Mohamed(25) kutoka jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Serengeti Allan Chonjo akiongea kwa njia ya sinu na moja wa washindi wa droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti iliyochezeshwa mapema leo jijini Dar es Salaam kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo. Ambapo
washindi wawili wamejishindia ‘Samsung tablets’ ambao ni Mwl. John Yesaya (49) kutoka mkoani Kilimanjaro na Salehe Mohamed(25) kutoka jijini Dar es Salaam.

Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo (kulia) akizungumza na wana habari (hawapo pichani) katika droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti, jijini Dar es Salaam.

Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo (kulia) akizungumza na wana habari (hawapo pichani) katika droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti, jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Serengeti Allan Chonjo akichezesha droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti iliyochezeshwa mapema jijini Dar es Salaam kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo na anayemshuhudia ni afisa Mwandamizi kutoka PWC (aliyesimama).

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Serengeti Allan Chonjo akichezesha droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti iliyochezeshwa mapema jijini Dar es Salaam kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo na anayemshuhudia ni afisa Mwandamizi kutoka PWC (aliyesimama).

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Allan Chonjo akitangaza washindi wa droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na kampuni hiyo nchini kote, kushoto kwake ni Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo, na kulia kwake ni Afisa Mwandamizi kutoka PWC Bwana Tumain iliyofanyika mapema jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Allan Chonjo akitangaza washindi wa droo ya kwanza ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inayoendeshwa na kampuni hiyo nchini kote, kushoto kwake ni Meneja wa bia ya Serengeti Rodney Rugambo, na kulia kwake ni Afisa
Mwandamizi kutoka PWC Bwana Tumain iliyofanyika mapema jijini Dar es Salaam.

MAWINDO ya safari ya Brazil inayolipiwa gharama zote sasa ni juu ya wateja wa bia ya Serengeti ambao wamepata wiki iliyojaa zawadi kemkem kutoka bia za bure, pesa taslim na ving’amuzivyakutosha. Asubuhi ya leo Kampuni ya Bia ya Serengeti imeendesha droo yake ya kwanza katika Kiwanda cha Bia cha Serengeti.

Droo iliyochezeshwa kiwandani hapo mapema leo, ilishuhudiwa na wanahabari, maofisa waandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, PWC, na Push Mobile. Promosheni hii ya kurudisha fadhila kwa wateja itaendeshwa kwa wiki 11 zijazo.
Katika droo ya kwanza ya Winda Safari yaBrazil na Serengeti wamepatikana washindi wawili wa (ipad) Mwl. John Yesaya (49) kutokamkoani Kilimanjaro na Salehe Mohamed (25) kutokajijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya simu ya kiganjani mshindi wa IPAD Salehe Mohamed (25) kutoka jijini Dar es Salaam, alishikwa na butwaa na kujiona mwenye bahati mara baada ya kutamkiwa kuwa ni mmoja ya mshindi wa IPAD kupitia kampeni hii. Washindi hao hawakutegemea kuwa miongoni mwa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni hiyo. Mshindi wa pili alielezea furaha yake na kuonekana kutoamini alichosikia.

Washindi wote wawili waliishukuru Kampuni Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwajali wateja wake siku zote na kuwatimizia mahitaji yao kwa kufanya vitu vya kustaajabisha kila kukicha alisema, Bw. Salehealisema “kwa kweli siamini, inanipa furaha na kujivunia kuwa mteja wa bia ya Serengeti. Kwa mimi kuwa mwenye bahati ya kupata (IPAD) ‘Samsung tablet’ inanipa ari kubwa hasa katika ulimwengu wa sasa wa dijitali.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Bw. Allan Chonjo alieleza kuwa promosheni iliyofunguliwa kwa wateja wote nchi nzima ambao wameshaanza kunufaika na kampeni hii. Zaidi ya wateja 172 wamejishindia fedha taslimu za kitanzania 5,000, na wateja 130 wamesha jishindia 10,000 ndani ya wiki hii ya kwanza ya promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti.
Wote hao wamepata zawadi zao kupitia njia ya simu ya kiganjani kwa kutuma maneno na tarakimu zilizopo chini ya kizibo kwenda namba 15317. Aliendelea kuelezea kuwa wateja wengi wameweza kufaidika zaidi kwani tangu uzinduzi wameweza kupata washindi wanne (4) waliojishindia ving’amuzi Robert M. Kitalikutoka Kilimanjaro, Deus P. Mwikitalu kutoka Buhongwa jijini Mwanza, Ali Hemed kutoka Mbezi jijini Dar es Salaam na Friimin R. Massawe kutoka Kilimanjaro.

Tunataka kuwakumbusha wateja wetu kuwa bado tuna zawadi za kutosha za kushindaniwa katika promosheni hii kubwa zaidi ni ile ya safari ya Brazil itakayolipiwa gharama zote. Pia tunatoa ving’amuzi na IPAD kwa wateja wetu cha kufanya ni wewe kufungua bia yako ya Serengeti kokote nchini na fuatilia maelezo ya promosheni na uweza kuwa mshindi wetu wa wiki inayokuja. Pia unaweza kufuatilia kupitia ukurasa wetu wa facebook www.facebook.com/serengetipremiumlager. Tumeanza vizuri hivyo hatunabudi kuwashukuru wateja wetu. “aliongeza Chonjo”

Kunywakwatahadhari. Inauzwakwawenyemiaka 18+