Mwinyi (picahni juu), aliyasema hayo jana jioni, alipotembelea maonyesho hayo huku akiwa ameambatana na Waziri Mkuu Mstaafu, Samwel Malicela, alisema taasisi yab Aga Khan imefanya mambo mengi nchini.
Alisema binafsi amebahatika kukutana na Imam Aga Khan zaidi ya mara mbili, ambapo zote amekuwa akizungumza mambo mengi ya maendeleo kuhusiana na Tanzania.
“Imam Aga Khan muda wote amekuwa na akisisitiza maslahi na mafanikio ya watanzania hayo yanatokana na kuwa na mapenzio mema na watanzania,” alisema.
Alisema jambo hilo ndio maana lilimfanywa kuwa mstari wa mbele katika kuboresha sekta ya elimu na afya, ambayo imekuwa tegemeo kubwa la watanzania kunufaika na huduma hizo.
Hivyo, alisema maonyesho hayo yameonyesha ni namna gani Aga Khan amekuwa akiisaidia nchi bila kujali dini, rangi au kabila yeye anachojari ni utu.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Taasisi ya Shia Ismailia Tanzania, Kamal Khimji alisema maonyesho hayo wanayatumia kuonyesha upendo na namna gani wanavyojitahidi kuisaidia wananchi.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akikaribishwa katika hafla ya Maonyesho ya picha kuhusu Taasisi ya Aga Khan, jana kwenye ukumbi wa Diamod Jubilee jijini Dar es Salaam.
Mzee Mwinyi akisalimia viongozi mbalimbali wa taasisi hiyo
Waakiendelea na mazungumzo kwenye chumba cha mapumziko.
Wageni ukumbini.
Mzee Mwinyi akiingia ukumbini na Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam.
Mzee Mwinyi akiwa ameketi meza kuu na viongozi wa Tasisi hiyo ya Aga Khan.
Makamu wa Rais wa Taasisi ya Aga Khan Tanzania, Kanal Khimj akitoa manano ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mzee Mwinyi kuzungumza
Mzee Mwinyi akizungumza; “Hekima ikiongezeka Maneno yanapungua”, akisema Mzee Mwinyi mwishoni mwa hotuba yake iliyojaa hekima. Imetayarishwa na theNkoromo Blog