Kasha la wimbo wa bongo tambarare kama linavyoonekana pichani
BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya, Ngoma Africa Band, aka ‘FFU’ imeanza shamra shamra za kusherehekea miaka 5O ya uhuru wa Tanzania mapema baada ya kutoa kibao chao kipya kinachojulikana kama Bongo Tambarare.
Ngoma Africa band wamestua ulimwengu kwa kurusha hewani wimbo huo mpya uliobeba jina la “Bongo Tambarare” kama mojawapo ya mwanzo wa shamra shamra za kuelekea katika sherehe za miaka 50 ya Uhuru!
Wimbo huo “Bongo Tambarare” utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda
Ras Makunja,akiimba kwa kushirikiana na Christian Bakotessa aka Chris-B, aka “Mshenzi” wa gitaa la solo, wimbo huo pia unasikika katika kambi ya FFU at www.ngoma-africa.com.
Wimbo huu ni salam za mwanzo tu kutoka bendi hiyo watanzania wote popote walipo, lakini bendi hiyo itaipua jikoni vitu vipya rasmi katika siku za usoni, hili kuhakikisha umma wa wananchi wa Tanzania na marafaki wote wanapata burudani kamili hisiyo na mfano. Usikose kusikiliza “Bongo Tambarare” ya watanzania at www.ngoma-africa.com