Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa somo kwa washiriki wa Semina ya siku tano ya Maadili na Jinsia inayolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari na watangazaji wa Redio za Jamii nchini iliyofadhiliwa na UNESCO kupitia mradi wa Demokrasia na Amani kuelekea uchaguzi 2015 inayoendelea mjini Dodoma.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya watangazaji na waandishi wa habari kutoka Redio mbalimbali za Jamii wakifuatilia mafunzo hayo yanayoendelea mjini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku tano yamefadhiliwa na Shirika la UNESCO kupitia mradi wa Demokrasia na Amani kuelekea uchaguzi 2015.
Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari na watangazaji wa redio za jamii wakichangia maoni kwenye mafunzo ya siku tano yanayoendelea mjini Dodoma.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka redio Triple A FM ya jijini Arusha Grace Damian akizungumzia changamoto mbalimbali zinazozikabili Redio za Jamii nchini.