Mashindano ya Mandela Open ChampionShip Yaanza Dar

Bondia Rashidi Samvu kutoka Kigoma (kushoto) akioneshana umwamba wa makonde na Hafidhi Kassimu wa Ngome wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela yaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.

Mgeni wa heshima na Diwani wa Kata ya Kawe, Othuman Kipete akiwa na viongozi wa Shirikisho la Mchezo wa Ngumi za Ridhaa nchini, Kutoka kulia ni Rais wa shirikisho hilo Mutta Rwakatare,   Makamu wa Rais, Lukelo Willilo na Mjumbe wa Maendereo ya Wanawake katika Mchezo wa Masumbwi nchini Aisha Vonialis.

Na Mwandishi Wetu

MASHINDANO ya mchezo wa Ngumi yanayotambulika kwa jina la Nelson Mandela Open ChampionShip yameanza kutimua vumbi katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam

Akizungumzia mashindano hayo yalivyo na ubora wa ali ya juu Makamu wa Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa nchini ‘BFT’ Lukelo Willilo ‘amesema mashindano hayo kwa sasa yameboleshwa kwa kufuata taratibu za chama cha ngumi za ridhaa Dunia kwa sasa mabondia awavai kofia ngumu wanakuwa vichwa wazi hivyo wapenzi wa ngumi weje waone mabadiliko makubwa katika ngumi za ridhaa ndio ambazo ni msingi wa maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini.

Alisema zamani mabondia walikuwa wanavaa kofia lakini kutokana na mabadiliko sasa awavai kofia wanapigana vichwa wazi ambapo kwa kuanzia tumeamua kuweka mashindano haya kwenye viwanja vya wazi na ni bule tu akuna kingilio ili kila mtu ajionee mabadiliko ya ngumi mashindano hayo yanayo husisha mikoa mbalimbali nchini

Aliongeza kuwa mashindano hayo yatakuwa ya siku tano kuanzia jumatano mpaka jumapili na ngumi zinanza kupigwa saa kumi na moja mpaka saa mbili usiku ngumi ndio zitakuwa zikisha. Katika ufunguzi huo bondia Patrck Kimweri wa Tanga alishindwa kufurukuta mbele ya Said Jabir wa ngome na Rashid Samvu wa Kigoma alipigwa kwa pointi na Hafidhi Kassimu wakati Fabian Gaudence akimsambalatisha Hussein Mnimbo.