KOCHA wa timu ya ngumi kutoka Mkoa wa Kigoma, Juma Lesso amesema timu yake ya mkoa huo imekuja imekamilika na ipo tayari kunyakuwa ubingwa wa ngumi katika mashindano ya wazi yatakayofanyika Feb 5, 2014 katika viwanja vya Tanganyika Pekazi vilivyopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya Mkoa wa Kigoma kushiriki katika mashindano makubwa kama hayo hivyo ina ari ya kutwaa ushindi na imeweka kambi yake maeneo ya Kawe ikijiandaa na mazoezi tayari kushiriki mashindano hayo yanayotaraji kuanza Februari 5.
“…Tuna mshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya kuhakikisha tunashiriki katika mashindano haya kwa mara ya kwanza,” alisema kocha Lesso.
Aliongeza kuwa timu hiyo ambayo imekuja na wachezaji 10 kati ya hawo wanawake watatu na wanaume saba ambao wakekuja kuwakilisha Mkoa wa Kigoma tutahakikisha kuwa tunachukuwa ubingwa huo ambao upo wazi
Lesso ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo aliwataja baadhi ya mabondia aliokuja nao kuwa ni Agnes Mushi, Ezira Josefu, Rashidi, Abasi na wengine ambao walikuwa katika kambi ya mkoa huu. “…Tumepewa sapoti kubwa na mkuu wa mkoa hivyo tutaakikisha atumwangushi na tunarudi na ubingwa kwani tumejipanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya juu kabisa.