NI kutambua mchango mkubwa, hii ni zawadi inayowafaa vinara! Tuzo ya ufanisi bora kabisa katika afya ya akinamama na watoto wachanga: Tuzo ya Mama Afrika imewadia. Watu wa kila kada, ikiwa ni pamoja na watoa huduma za afya, watoa maamuzi, viongozi katika jamii na wanaharakati wanaojishughulisha na uhai wa akinamama, na watoto katika jamii zao; Jitihada zao zimeokoa na zimesaidia kuwepo kwa kizazi chenye afya na furaha barani Afrika. Kwa kutambua mchango wao mkubwa CARMMA, ambayo ni kampeni ya Umoja wa Afrika Kupunguza vifo vya akinamama na watoto wachanga, imezindua Tuzo ya Mama Afrika.
Tuzo hii iliyoandaliwa na Umoja wa Africa kwa kushirikiana na Mama Ye!, itawatambua mashujaa wa kweli kutoka bara zima la Afrika. Itatambua mchango mkubwa wa mtu mmoja mmoja, jamii, makampuni, serikali au mashirika ambayo huhakikisha akinamama na watoto wachanga wa Afrika wanakuwa hai tena kwa afya njema. Ni tuzo ya heshima na hadhi ya juu barani Afrika kwa kutambua mchango mkubwa wa wadau wa masuala ya afya ya akinamama na watoto wachanga.
Tuzo hii itakuwa na maeneo sita
• Ugunduzi katika masuala ya kifedha
• Upatikanaji wa huduma
• Ushirikishi wa wanajamii
• Makundi ya pembezoni na mazingira magumu
• Maeneo ya Vita na hali hatarishi
• Kujengea uwezo
Tuzo ya Mama Afrika imepewa jina kwa heshima ya Mama Miriam Makeba, mwimbaji maarufu aliyewahi kupewa uraia katika nchi 10 za Afrika kwa kutambua ushiriki wake katika kupinga ubaguzi wa rangi, na pia binti yake alifariki kutokana na matatizo wakati wa ujauzito.
Bw Nelson Lumumba Lee, mjukuu wa Miriam Makeba alimzungumzia bibi yake kuwa ni “mtu aliyejali sana afya ya watoto na akinamama na aliamini kuwa wanawake ndio walezu wa taifa”.
Inaweza kuwa ni taasisi ambayo imeleta mabadiliko makubwa katika huduma wanazopata akinamama na watoto wachanga, au serikali ambayo imewekeza pesa na rasilimali kwenye huduma za afya ya mama na watoto. Au anaweza kuwa ni mtu ambaye ametoa huduma kwa miaka mingi, na hasa katika mazingira magumu sana ili tu akinamama na watoto waweze kuvuka salama kipindi cha kujifungua. Wote hawa wanahitaji kutambuliwa.
Kwa Tanzania, unaweza kumpendekeza mtu au taasisi kwa tuzo hii kwa kujaza fomu hii. Kwa taarifa zaidi fuata kiuganishi hiki http://www.carmma.org/update/mama-afrika-award au barua pepe info@carmma.org.
Kwa taarifa zaidi ingia hapa:- http://bit.ly/1dy8i5h