Mahakama Rombo Yawafunga Maisha Wawili kwa Kulawiti Wanafunzi

Jaji Mkuu Tanzania, Chande Othuman

Jaji Mkuu Tanzania, Chande Othuman

Yohane Gervas Rombo

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Rombo imemhukumu Jacobo Simon maarufu kama babu suzuki (62) mkazi wa Kijiji cha Mriyahe Ubetu Tarafa ya Usseri Wilaya ya Rombo kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti binti mwenye umri wa miaka nane na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.

Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Rombo, Charles Myombo alisema kuwa Simoni amepewa adhabu hiyo baada ya kuridhishwa pasipo na shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Aidha Myombo alisema kuwa adhabu hiyo itakuwa fundisho kwawe pamoja na watu wengine wenye tabia kama hiyo ambayo sasa inaonekana kushamiri katika maeneo mbalimbali ya nchi. Awali mwendesha mashtaka alidai mahakani hapo kuwa mshtakiwa alikuwa na mazoea ya kufanya unyama huo zaidi ya mara nne kwa binti huyo ambaye jina lake linahifadhiwa. Alisema mnamo mwezi Septemba 2010, na Desemba 2011 pamoja na November 2012 mshatakiwa alikuwa akimlawiti binti huyo na Aprili 24 2013 majira ya
saa kumi jioni ilibainika.

Alisema mama wa binti huyo alimwona mwanae akitokwa na kinyesi sehemu za siri na alipomuuliza binti huyo alianza kuelezea kilichotokea na ndipo na ndipo waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata.

Aidha Hakimu Myombo alisema uchunguzi wa daktari unaonesha kuwa binti huyo ameathirika vibaya sehemu zake za siri hali inayomfanya kutokwa na kinyesi muda wote na hivyo binti huyo ambaye ni
mwanafunzi wa darsa la nne kwa sasa anavaa pempasi muda wote.

Wakati huo huo mahakama hiyo pia imemhukumu kifungo cha maisha mtu mwingine aliyefahamika kwa jina la John Izioka 40, mkazi wa Chumvini Kenya kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wa Darasa la pili jina limehifadhiwa.