Sherehe za Miaka 50 Mapinduzi Zanzibar Zafana , Dk Shein Atangaza Mapumziko Kesho

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la  vikosi vya ulinzi katika kilele cha miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, huko uwanja wa Amaan leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la  vikosi vya ulinzi katika kilele cha miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, huko uwanja wa Amaan leo.

Vingozi mbali mbali wa Kitaifa na Mataifa wakisimama kupokea salamu ya Heshma iliyotolewa na Vikosi vya Ulinzi wakati wa Sherehe za Kilele cha miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar katikaUwanja wa Amaan Mjini Unguja.

Wananchi na Viongozi waliohudhuria katika sherehe za kilele cha Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ziliaofamyika le katika uwanja wa Amaan. [Picha zotea na Ramadhan Othman, Ikulu.]

Wananchi na Viongozi waliohudhuria katika sherehe za kilele cha Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ziliaofamyika le katika uwanja wa Amaan. [Picha zotea na Ramadhan Othman, Ikulu.]

Sherehe za Miaka 50 Mapinduzi Zanzibar Zafana , Dk Shein Atangaza Mapumziko Kesho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma ya vikosi vya ulinzi katika kilele cha miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, huko uwanja wa Amaan leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma ya vikosi vya ulinzi katika kilele cha miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, huko uwanja wa Amaan leo.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
SHEREHE za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanyika leo mjini Unguja katika Uwanja wa Aman huku zikishirikisha viongozi anuai wa kitaifa na kimataifa walioongozwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk. Mohamed Ali Shein.
Sherehe hizo zilizoambatana na maonesho mbalimbali ya shughuli za ulinzi na usalama na kijeshi pamoja na uchumi zilikuwa kivutio kikubwa kwa wananchi waliohudhuria katika sherehe hizo.
Maonesho yaliokuwa na mvuto zaidi katika sherehe hizo ni gwaride la askari wa zamani kutoka vikosi vya wakoloni ambalo lilionesha namna gwaride lilivyokuwa likiendeshwa kwa mbwembwe na hata askari anapokosea ndani ya gwaride papo hapo alipewa adhabu huku wenzake wakiendelea.
Kikosi kingine kilichokuwa na mvuto zaidi ni kile cha askari wa jeshi la ukombozi ambacho kiundwa na askari wa kikosi hicho wa zamani ambao walikuwa wazee huku wakionesha uwezo wa kutembea kwa ukakamavu chapo wa shida kutokana na umri wao.
Vikosi vingine vilivyokuwa na uvuto ni kikosi cha makomandoo wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania (JWTZ) kilichoonesha namna ya kupambana na adui kwa kutumia ujuzi wa mwili bila silaha na baadaye kutumia silaha za visu na vifaa vingine.
Kikosi hicho pia kilikuwa na mvuto zaidi baada ya makomandoo hao kuonesha ujuzi wa kuvunja vitu vizito kama matofari, mbao, fimbo na uvumilivu wa kujihami na maadui wakiwa na silaha anuai katika mapambano.
Aidha, mbali na kufanyika gwaride la heshima kwa mgeni rasmi likijumlisha vikosi anuai vya ulinzi na usalama pia vikosi vya JWTZ, Jeshi la Polisi, na Vikosi vya JKU na KMKM vilipita kuonesha shughuli zao anuai wawapo kazini.
Maonesho mengine yaliofanyika katika maadhimisho hayo ni halaiki ya watoto kutoka shule za msingi maeneo mbalimbali, ambao pia walionesha sarakasi na sura za vitabu kwa maumbo na maandishi anuai uwanjani hapo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Rais wa Zanzibar, Dk. Shein alijivunia mafanikio anuai ya kimaendeleo yaliopatikana katika Nyanja mbalimbali ambayo ni matunda ya kipindi chote tangu mapinduzi hayo.
Dk Shein pia ametangaza kesho jumatatu kuwa siku ya mapumziko kwa Tanzania Bara na Zanzibar ikiwa ni ishara ya kupumzika kujivunia mafanikio na kujiandaa kufanya kazi kwa nguvu mpya na bidii kuleta mafanikio zaidi kwa kipindi hiki kipya cha miaka 50 ya Mapinduzi.
Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar pia zilihudhuriwa na Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, marais wa Comoro na Uganda, Makamu wa Rais Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengi Pinda, Makamu wa Kwanza na wa pili wa Rais wa Zanzibar, mabalozi wa nchi mbalimbali, viongozi wawakilishi wa nchi.
Wengine ni viongozi wa Serikali zote mbili, maras wastaafu wa SMZ, viongozi wakuu wa mashirika ya kimataifa na viongozi wa vyama na asasi anuai, na viongozi wastaafu wa serikalini zote mbili kitaifa na wananchi.
Miradi ya maendeleo ipatayo 114 imezinduliwa katika kipindi chote cha maandalizi kabla ya kufikia maadhimisho rasmi ya serehe hizi yaliyofanyika leo.