MAJESHI ya Lebanon yametangaza kuwa kamanda wa cheo cha juu wa kundi la kigaidi la Al Qaeda katika nchi hiyo Majid Al – Majid amekufa akiwa kizuizini. Kamanda huyo ambaye ni raia wa Saudi Arabia, alikuwa kiongozi wa kundi la Abdulha Azzam ambalo lina uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda, ambalo pia limekuwa likikiri kuendesha mashambulizi ya kigaidi na milipuko ya mabomu kulenga maeneo yanayokaliwa na waumini wa madhehebu ya Shia katika siku za hivi karibuni.
Miongoni mwa mashambulizi waliyokiri kuhusika nayo ni shambulizi katika Ubalozi wa Iran nchini Lebanon. Maofisa wa jeshi wanasema Al Majid amekufa kutokana na maradhi ya figo na kwamba hali yake ilikuwa imezorota kwa muda sasa. Al Majid alikamatwa mwezi uliopita na alikuwa akishikiliwa katika kizuizi cha siri.
-BBC