WAZIRI wa Fedha nchini Tanzania, Dk. William Mgimwa amefariki dunia nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata na kuthibitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Omben Sefue Mgimwa amefariki leo majira ya saa tano na dakika 20 nchini Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Akizungumza na moja ya vyombo vya habari, Sefue alisema Gimwa amefariki dunia nchini Afrika Kusini alipokuwa katika matibabu. Hata hivyo hakufafanua zaidi Waziri Mgimwa amefariki dunia kwa ugonjwa gani. Akifafanua zaidi alisema taratibu za kusafirisha mwili wa Dk. Mgimwa kuja Tanzania kwa ajiri ya mazishi zinafanywa na ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini. dev.kisakuzi.com inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote wa msiba wa kiongozi huyo wa Taifa. dev.kisakuzi.com itawaletea taarifa zaidi za msiba huo hapo baadaye.